RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI...YUMO MWENYEKITI MPYA WA TUME YA UCHAGUZI (NEC), BODI YA MIKOPO (HESLB)


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Jaji Jacob Casthom Mwambegele aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Jaji Mwambegele anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Semistocles Kaijage ambaye amemaliza muda wake.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu amethibitisha hayo kupitia taarifa aliyoitoa leo Desemba 27,2021.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,pia Rais amemteua Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa mjumbe wa tume hiyo.

Jaji Kwariko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Jacob Casthom Mwambegele.

Mheshimiwa Rais Samia pia amemteua Jaji Sam Mpaya Rumanyika, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa hiyo imeeleza pia Rais amemteua Profesa Khamis Dihenga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB). Kabla ya uteuzi huo Profesa Dihenga alikuwa anahudumu kwa Mkataba katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro.


Profesa Dihenga anachukua nafasi ya Profesa William Anangisye aliyemaliza muda wake.


Rais Samia pia amemteua Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Mussa Muhidin Kissaka, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ambapo uteuzi huo umeanza Desemba 23, 202.1

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments