Klabu ya Simba Sc imeiathibu mvua ya magoli timu ya KMC FC kwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC uliochezwa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mjini Tabora.
Post Top Ad
Friday, December 24, 2021
SIMBA SC YAZIDI KUISOGELEA YANGA, YAINYUKA KMC FC 4-1
**************
NA EMMANUEL MBATILO
Simba Sc ilianza kupata bao la mapema kabisa kupitia kwa Beki wao kisiki Mohammed Hussein na baadae bao la pili likifungwa na Onyango na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza Simba Sc ikionekana bado ikiwa na hamu ya kuongeza mabao mengine kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na hisia kubwa kwa mashabiki wake.
Kibu Dennis tuseme ndiye nyota wa mchezo kwani licha ya kucheza kandanda safi uwanjani aliweza kupachia mabao mawili yaani la tatu na la nne kwenye mchezo huo huku mashabiki wakimshangilia kwa shangwe hasa kwa kufurahishwa na kiwango chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Author Details
Malunde 1 blog ni blog ya Kiswahili maarufu duniani kwa habari za Matukio, Siasa, Magazeti, Nyimbo za asili na habari za kusisimua.
No comments:
Post a Comment