RAIS MWINYI AMTEUA CHARLES HILARY KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Charles Hilary Mkurugenzi Mteule wa Idara ya Mawasiliano, Ikulu Zanzibar
***
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wafuatavyo;

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua Charles Martin Hilary kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.


Pili kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said leo Desemba 30,2021 pia Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua Yusuph Majid Nassor kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua Dkt. Idrissa Muslim Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi Uhaulishaji Ardhi Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza leo Desemba 30,2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments