NIC YAKABIDHI VITI VITANO (WHEELCHAIR) NA MAFUTA KWA WATU WENYE ULEMAVU

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Karimu Meshack (katikati) akikabidhi msaada wa mafuta ya kupaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wakati walipofika katika kituo cha Haki sawa cha watu wenye ulemavu Mabibo jijini Dar es Salaam. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Karimu Meshack akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa viti vitano vya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na mafuta ya kupaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wakati walipofika katika kituo cha Haki sawa cha watu wenye ulemavu Mabibo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Meneja Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Karimu Meshack ambaye aliambatana na watumiishi wngine wa shirika hilo kwaajili ya kutoa msaada wa viti vitano vya watu wenye ulemavu wa viungo pamoja na mafuta kwaajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Kaimu Mwenyekiti wa Kituo Haki sawa cha watu wenye ulamavu Bw.Hilaly Gatunga akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa viti vitano vya watu wenye ulemavu pamoja na mafuta kwaajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakipata picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kituo cha Haki sawa cha watu wenye ulamavu mara baada ya kukabidhi msaada wa viti vitano vya watu wenye ulamavu wa viungo na mafuta kwa watu wnye ulemavu wangozi

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Bima la Taifa (NIC) wamekabidhi msaada wa viti vitano kwa watu wenye ulemavu pamoja na mafuta kwa watu wenye ulamavu wa ngozi katika kituo cha Haki Sawa kwa watu wenye ulemavu kilichopo Mabibo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Meneja Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Karimu Meshack amesema wamefanya utafiti katika kutekeleza sera yao ya kurudisha kwa jamii wakagundua kwamba watu hao wanachangamoto ya vitimwendo na mafuta hivyo wameamua kuwapatia ili waweze kutiimiza majukumu yao.

"Mtanzania ambaye anatembea kwa mikono maana ake kwamba anashindwa kutimiza shughuli zake za kila siku za kiuchumi, anashindwa kutafuta mahitaji yake ya kila siku kwasababu ya mazingira yake ya kutembea". Amesema Bw.Meshack.

Amesema wenye ulamavu wa ngozi wanahitaji kwenda kwenye majukumu yao lakini mionzi inampa shida katika kutekeleza majukumu yake yya kila siku hivyo basi wamewaleteaa mafuta ili kutatua changamoto zao za afya lakinni wametatua changamoto zao za kujipatia kipato na shughuli za kiuchumi za kila siiku.

Ametoa wito kwa taasisi zingine za Serikali pamoja na na taasisi binafsi kuwakumbuka watu wenye ulemavu kwa kutatua changamoto zao za kila siku hasa pale wanapokuwa katika majukumu yao.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kituo Haki sawa cha watu wenye ulamavu Bw.Hilaly Gatunga amesema huduma walizopata kuttoka NIC wamefurahishwa kwa kuweza kuwakumbuka kwa kuwaletea msaada wa vifaa ambavyo vitaweza kuwasaidia kutatua changamoto ziinazowakbili walemavu.

Ameomba baadhi ya makampuni, Taaisisi na mashirika kuwa na moyo wa huruma kwa kuwasiaida watu wenye ulamavu kwa kutatua changamoto zao kwa ujumla.

Pamoja na hayo ameaomba watu wa usalama kujaribu kutoa elimu kwa baadhi ya madereva hasa katika maeneo ya zebra kuweza kuheshimu alama hizo pale wanapopita watu wenye ulemavu wakivuka barabara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments