KATIBU MKUU KILIMO ATOA MIEZI MIWILI KUKAMILISHWA KWA UJENZI WA MAABARA YA SUMU KUVU KIBAHA



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo Andrew Masawe akimzikiliza Casmir Tobange Mhandisi Mshauri wa Ujenzi wa Mradi wa Maabara ya uchunguzi wa Sumu Kuvu iliyopo Kibaha mkoani Pwani wakati alipotembelea na kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa maabara hiyo.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo Andrew Masawe na ujumbe wake wakikagua ujenzi wa jengo hilo la maabara.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo Andrew Masawe akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri wa mradi huo Mhandisi Casmir Tobange wakati alipokagua mradi huo.
Mhandisi Mshauri wa mradi huo Mhandisi Casmir Tobange akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika mradi huo.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo Andrew Masawe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mradi huo.
Moja ya eneo la mradi huo linavyoonekana wakati ujenzi ukiendelea.

....................................

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo Andrew Masawe ametoa miezi miwili kwa Mkandarasi anayejenga maabara ya udhibiti wa sumu kuvu iliyopo Kibaha Mkoani Pwani kukamilisha ujenzi wa kituo hicho ili kiweze kuanza majukumu yake.

Akizungumza wakati wa ziara yake na kamati ya ujenzi wa mradi unaogharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.8, Masawe amesema kuna kila sababu ya mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ili aweze kukamilisha haraka huku hadi sasa ujenzi huo ukiwa umefikia asilimia 50 badala ya 86 zilizokuwa zimetarajiwa.

Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa ujenzi wa maabara hiyo kuharakishwa kutokana na umuhimu wake ikizingatiwa kuwa fedha zote kwa ajili ya utekelezaji wake zimeshatolewa hivyo haupaswi kuwa na visingizio vyovyote.

"Nilitoa maelekezo kuwa miradi hii lazima ifuatiliwe sana, ilipaswa tuwe tumefikia asilimia 86 lakini sasa tupo na asilimia 50, itawalazimu kufanya kazi usiku na mchana ili mradi huu huweze kukamilika"alisema Masawe

Aidha amesema licha ya kuchelewa kwake kwa kiasi kikubwa ameridhishwa na ubora wa jengo hilo huku akimtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anaongeza idadi ya vibarua ili kuchagiza kasi ya ujenzi huo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa udhibiti wa sumu kuvu Clepin Josepht amesema mbali na jengo hilo linalotarajiwa kuwa na vifaa vya kisasa vya upimaji wa sumu kuvu, chini ya mradi huo pia wanatekeleza ujenzi wa vituo mbalimbali vya upimaji wa sumu kuvu hiyo.

Amesema chini ya ushirikiano wa Serikali na wafanyadhili wa mradi huo ambao ni Benki ya Afrika, kimetengwa kiasi cha Sh Bilioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa vituo mbalimbali vya upimaji wa sumu kuvu katika wilaya 18 za Tanzania bara na Visiwani, lengo likiwa kukabiliana na hali hiyo.

" Kupitia mradi huu pia kwa kushirikiana na wenzetu kutoka Shirika la Viwango Tanzania(TBS) tumeweza kutoa elimu kwa watu zaidi ya 500 wakiwemo wafanyabiashara kwa ajili ya kupambana na tatizo hili" amesema Josephat

Aidha ameitaka jamii hususani wafanyabiashara kujenga mazoea ya kufanya uchunguzi wa mazao yao kabla ya kuyaingiza sokoni ili kupunguza uwezekano wa watu kupatwa madhara yatokanayo na sumu kuvu.

Na Mwandishi Wetu, SERIKALI imesema haijazuia mfanyabiashara yeyote kuuza mazao yake nje ya nchi, na kwamba mkulima wa nchi hii wajibu wake ni kulima , kuvuna ,kuhifadhi na kuuza kwa kuwa hiyo ndio biashara yake.

Akizungumza katika ziara ya kikazi wilayani Mpanda mkoani Katavi baada ya kukagua , kituo cha kununulia mahindi cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali haijazuia uuzaji wa mazao nje ya nchi.

"Hivyo kama yupo ambaye amazuiwa kuuza mazao yake nje ya nchi Wizara hiyo inamkaribisha na watampa ushirikiano kwani vibali vyote vya kusafirisha mazao nje ya nchi wanatoa vibali bure ili mradi awe leseni ya kufanya biashara

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments