CHUI AVAMIA DARASA, AJERUHI MWANAFUNZIChui mmoja alikamatwa katika mji wa kaskazini wa India Aligarh baada ya kuingia katika shule moja na kumshambulia mwanafunzi.


Mwanafunzi huyo , ambaye alipata majeraha madogo alisema kwamba alitoroka katika darasa hilo baada ya kumuona mnayama huyo akiwa amejificha.

Chui huyo mwenye umri wa miaka mitano baadaye alitulizwa na kukamatwa baada ya juhudi za saa kumi na moja.


Maafisa wanasema kwamba Chui huyo kutoka msitu jirani huenda alipotea njia na kuingia katika shule hiyo .

Mizozo kati ya chui na binadamu huwa jambo la kawaida nchini India huku Chui hao wakilazimika kutafuta chakula katika vijiji na miji.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments