AGGY BABY AACHIA WIMBO MPYA "KAMNYWESO" - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, December 14, 2021

AGGY BABY AACHIA WIMBO MPYA "KAMNYWESO"


Na Mwandishi Wetu.

MALKIA  kwenye muziki wa Bongo fleva Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby ametambulisha rasmi wimbo wake mpya wa Kamnyweso wenye mtindo wa Amapiono aliomshirikisha msanii Stompion.

Aggy Baby ameachia rasmi 'Audio' ya Kamnyweso mapema 13 Desemba 2021 ukiwa unapatikana karibu kwenye 'platform' zote za muziki za mitandaoni ikiwemo Boomplay, Youtube,  iTunes,  Audiomack na zingine nyingi.

"Fans wangu na wadau wote wanaweza kuusikiliza wimbo wangu mpya kupitia mitandao karibu yote.
Ikiwemo Google play, TIDAL, Amazon na sehem zingine ikiwemo kwenye mitandao yangu ya kijamii kwa jina la @aggybaby_"  Alisema.

Wimbo huo wa 'Kamnyweso' pia unaweza kuupata kupitia link hii: https://youtu.be/ERw_PyZxGGE

Au kufuatilia kupitia kurasa zake 'page' za instagram Aggybaby_  ( https://instagram.com/aggybaby_?utm_medium=copy_link )

Aggy Baby pia bado yupo kwenye chati za muziki akitamba na nyimbo zake kama: 'WATAJUAJE', 'WANIPA' na nyingine.

Kamnyweso ni aina ya pombe kama unavyosema gongo ama denge.

Aggy Baby mbali ya kuimba pia ni rapa (Rapper),  msanii wa filamu (Actor), mtunzi na Mwandishi wa nyimbo na Mwanaharakati wa Vijana katika mambo ya kusaidia jamii.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages