MSIGWA : WAANDISHI WA HABARI MMENIONESHA HESHIMA KUBWA...MMENISTIRI SANA

Msemaji mkuu wa Serikali na Mkuu wa Idara ya habari-Maelezo Gerson Msigwa 

Na Dotto Kwilasa - Malunde 1 blog Dodoma

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Idara ya habari-Maelezo Gerson Msigwa amewashukuru Waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kwa juhudi na ufanisi waliouonyesha kwa kipindi chote cha ratiba ya mikutano ya Mawaziri na vyombo vya habari uliolenga kuelezea mafanikio ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara.


Mikutano hiyo iliyokuwa inaratibiwa na Idara ya habari-Maelezo ilianza rasmi mara baada ya uzinduzi wa nembo ya Miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara Novemba 1,2021 na kuhitimishwa rasmi Novemba 30,2021 na kuwawezesha wananchi kuijua vyema Tanzania.


Akiongea wakati wa kufunga Mkutano huo Msigwa alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wanahabari  kwa kujitoa kuhabarisha jamii kwa utulivu mambo muhimu ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara ambapo jumla ya  wizara 23 ziliweza kueleza mafanikio yao kuelezea hisia zake kuwa amesitirika.


"Nasikia furaha,mmenionesha heshima kubwa kwa utulivu wenu,kwa siku zote 30 mlizokaa hapa wananchi wamepata fursa ya kutafakari kwa pamoja kuijua nchi yetu kwa undani zaidi tangu tulipotoka,tulipo na tunapoelekea,niseme ukweli wa dhati ya moyo wangu mmenistiri sana",amesema Mkurugenzi huyo wa Idara ya habari-Maelezo.


Amesema katika mikutano hiyo Waandishi wa Habari walipewa fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao Kisha  mawaziri kutajibu na kuyatolea ufafanuzi maswali yote.


"Tumemaliza salama ,imani yetu kama Serikali wananchi wameelimika na watauenzi zaidi uhuru tulio nao,kupitia  mahojiano maalum kati ya vyombo vya habari na viongozi mbalimbali wa Serikali walioko madarakani na wastaafu na watu mashuhuri, Sekta binafsi na wananchi kila mwananchi amepata uelewa,"amesema .


Katika hatua nyingine Msigwa ameeleza kuwa Idara hiyo ya habari itatumia hotuba hizo za Mawaziri  kuandaa machapisho,majarida mbalimbali na Makala ya saa moja yenye mjumuisho wa vipindi vya miaka 60 ya uhuru ili kuwapa nafasi watanzania  kujionea mafanikio yaliyofanywa na Serikali kwa awamu zote za viongozi wakuu wa nchi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments