WAZIRI SIMBACHAWENE ALITAKA JESHI LA POLISI KUMHOJI ASKOFU JOSEPHAT MWINGIRA


Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. George Simbachawene

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. George Simbachawene, amemtaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, kumtafuta na kumhoji Askofu Josephat Mwingira ili kusaidia kupata ukweli zaidi wa tuhuma nzito alizozitoa.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 27, 2021, baada ya taarifa mitandaoni zikieleza kuhusu tuhuma alizozitoa Askofu Mwingira kuhusu masuala ya mali zake na kunusurika kuuawa mara tatu.

"Tamko la Askofu Mwingira na mimi nimelisikia kwenye mitandao ni tuhuma nzito sana, kama haya matukio ni ndivyo yalitokea kwanini alikuwa hatoi taarifa polisi ili wahusika watafutwe, na yote yatokee wewe uko salama tu na baadaye unangojea mwisho wa mwaka na unasukuma lawama, kama aliyoyasema ni kweli tutahitaji atusaidie kutupa taarifa zaidi,”amesema Waziri Simbachawene.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments