MWANAFUNZI AFIA KWA MWENDESHA BODABODA WALIYEKUTANA FACEBOOK - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Wednesday, December 22, 2021

MWANAFUNZI AFIA KWA MWENDESHA BODABODA WALIYEKUTANA FACEBOOK
JESHI la Polisi nchini Kenya wanamshikilia Dereva Bodaboda kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Thaara ambaye walikutana nae Facebook.

Polisi wanasema wawili hao walikutana Facebook na kuanzisha urafiki na Mwanafunzi akasafiri kutoka Kijiji cha Kamahuha na akamfuata Mwanaume nyumbani kwake eneo la Gaturi ambako umauti umemkutia.

“Mwili utafanyiwa uchunguzi kujua kilichopelekea kifo cha mwanafunzi huyo, na tayari tunaendelea kuwahoji Majirani ambao wamekiri kumuona Mwanafunzi akiingia ndani kwa Bodaboda huyo,” imesema Polisi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages