THPS YATOA MSAADA WA MAGARI KUONGEZA KIWANGO CHA UTOAJI CHANJO YA UVIKO - 19 NA HUDUMA ZA UKIMWI SHINYANGA


Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory  (kushoto) akimkabidhi funguo za magari matatu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) limetoa msaada wa magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Magari hayo yamekabidhiwa leo Alhamisi Novemba 4,2021 na Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory amesema THPS ambayo inajihusisha na huduma za maambukizi ya VVU na UKIMWI na Matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI imetoa magari hayo ili yatumike katika shughuli za utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na Huduma za VVU na UKIMWI.

“THPS hivi sasa inafanya kazi zilizokuwa zinafanywa Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) katika wilaya zote mkoani Shinyanga, hivyo tunakabidhi magari haya ili yatumike katika masuala ya VVU na UKIMWI pamoja na utoaji chanjo ya UVIKO – 19”,amesema Anatory.

“Katika kikao chetu cha THPS na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga tulisema tutatoa magari lakini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy alijipambanua kuchangamkia fursa na kuomba magari kwa matumizi ya Halmashauri yake, hivyo kati ya magari haya matatu aina ya Landcruiser moja tumeipatia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na mengine yataenda Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT)”,amesema Anatory.

Katika hatua nyingine amesema THPS inatekeleza miradi ya VVU na UKIMWI na UVIKO – 19 katika mikoa ya Pwani, Shinyanga na Kigoma kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).

Akipokea magari hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary ameishukuru THPS kwa msaada huo wa magari kwa ajili ya shughuli za chanjo ya UVIKO – 19 na Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga.

“Tunawashukuru kwa msaada huu wa magari, tutayatunza ili kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafikia wananchi kama ilivyokusudiwa. Naomba wadau muendelee kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii”,amesema Zuwena.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO -19 na kuwapuuza baadhi ya watu wanaopotosha kuhusu chanjo hiyo kwani chanjo ni salama hakuna mtu aliyepata madhara baada ya kuchanjwa.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema magari hayo yaliyotolewa na THPS yataongeza kiwango cha utoaji chanjo ya UVIKO -19 kwa jamii pamoja na utoaji wa huduma za UKIMWI na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy ameishukuru THPS kwa kufanyia kazi ombi lake la kupatiwa gari huku akiahidi kuendelea kuimarisha mahusiano, ushirikiano na taasisi /mashirika mbalimbali ili kuwaletea maendeleo wananchi na kuinua mapato ambapo tangu aingie katika halmashauri hiyo ameinua mapato ya halmashauri kutoka Milioni 204 hadi Milioni 478.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary akizungumza leo Alhamisi Novemba 4,2021 wakati Shirika la THPS likikabidhi magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary akizungumza leo Alhamisi Novemba 4,2021 wakati Shirika la THPS likikabidhi magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya masuala chanjo ya UVIKO -19 na  UKIMWI. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory akizungumza leo Alhamisi Novemba 4,2021 wakati akikabidhi magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza leo Alhamisi Novemba 4,2021 wakati Shirika la THPS likikabidhi magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya masuala chanjo ya UVIKO -19 na  UKIMWI.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akilishukuru Shirika la THPS kwa kufanyia kazi ombi lake kuipatia gari Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo ameahidi kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa gari aina ya Landcruiser kwa masuala chanjo ya UVIKO -19 na  UKIMWI.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory  (wa pili kushoto) akimkabidhi Hati ya Nyaraka za makabiadho ya magari Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile. Shirika la THPS limekabidhi magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory  (kushoto) akimkabidhi funguo za magari Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary. Shirika la THPS limekabidhi magari matatu aina ya Landcruiser katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) kwa ajili ya kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la THPS, George Anatory  ( wa pili kushoto) akimkabidhi funguo za magari Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary.
Muonekano wa magari matatu aina ya Landcruiser yaliyotolewa na Shirika la THPS kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) yatumike kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Muonekano wa magari matatu aina ya Landcruiser yaliyotolewa na Shirika la THPS kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) yatumike kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Muonekano wa magari matatu aina ya Landcruiser yaliyotolewa na Shirika la THPS kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kamati ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) yatumike kuongeza kiwango cha utoaji Chanjo ya UVIKO - 19 na utoaji wa Huduma za UKIMWI na Matunzo kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment