TET YAPOKEA MAONI YA WADAU WA ELIMU JUU YA UBORESHAJI WA MITAALA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba akizungumza wakati wa uwasilishaji wa mada juu Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu kwa wahadhiri na wanafunzi wa Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wadau wa Elimu wakitoa maoni yao mara baada ya kuwasilishwa kwa mada juu Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu kwa wahadhiri na wanafunzi wa Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wadau wa Elimu wakitoa maoni yao mara baada ya kuwasilishwa kwa mada juu Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu kwa wahadhiri na wanafunzi wa Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wadau wa Elimu wakitoa maoni yao mara baada ya kuwasilishwa kwa mada juu Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu kwa wahadhiri na wanafunzi wa Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia uwasilishaji wa mada juu Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu kwa wahadhiri na wanafunzi wa Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba (wa pili kutoka kulia waliokaa)akipata picha ya pamoja na wadau wa elimu wakati wa uwasilishaji wa mada juu Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu kwa wahadhiri na wanafunzi wa Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imekutana na wahadhiri na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha mtaala na kupokea maoni yao juu ya nini kiboreshwe kjwenye mtaala.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho kilichofanyika hapo jana tarehe 24 Novemba 2021, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt.Aneth Komba amesema wameyapokea maoni ambayo wataenda kuyafanyia kazi na kuweza kuhakikisha malalamiko yanapungua kwa wadau wa elimu nchini.

"Tumeamua kufanya hivi kwasababu kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau kwamba mtaala wetu hautoi wanafunzi ambao wanaweza kujiajiri au kuajiriwa kumudu maisha yao". Amesema

Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya msingi, Bi. Zaituni Litanda ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam amesema ni vyema kurudisha mfumo wa zamani wa wanafunzi kwenda kidato cha kwanza kwa kufaulu na si kuchaguliwa huku akibainisha kuwa si lazima wanafunzi wote wafaulu.

Amesema katika shule aliyofundisha yeye wanafunzi wote wamefaulu mtihani wa darasa la saba lakini anatambua kuwa wapo baadhi ya watoto ambao walitakiwa kwenda kusoma cherehani na wengine ufundi wa magari kutokana na uwezo wao.

"Lakini wanaenda Sekondari sijui wanaenda kufanya nini. Hili litafanya tuendelee kupata wataalamu ambao hawakidhi vigezo na hawatakuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira," amesema Zaituni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments