TBS YAANDAA MAFUNZO KWA WADAU WA VIPURI VYA MAGARI NA KARAKANA


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya (katikati) akifungua mafunzo kwa wadau wa vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini yenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika.Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akifungua mafunzo kwa wadau wa vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini yenye yenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika.Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika mafunzo kwa wadau wa vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini lenye yenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika.Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Bw.Hamisi Mwanasala akizungumza katika mafunzo kwa wadau wa vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini yenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika.Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na TBS kuhusu vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini yenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika..Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la viwango Tanzania (TBS) imeandaa mafunzo kwa wadau wa vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini yenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Jijjini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema watumiaji hutegemea waagizaji na wauzaji wa vipuri vya magari na wenye karakana ili wawashauri juu ya aina na ubora wa vipuri sahihi kwa magari yao.

"Ikiwa mtumiaji hawezi kupata vipuri vyenye ubora na sahihi kwa mahitaji ya gari lake, hii inasababisha kuwepo kwa malalamiko juu ya thamani ya maisha yao na fedha zao". Amesema Dkt.Ngenya.

Amesema yapo baadhi ya magari baada ya kukaguliwa na kupimwa yanagundulika kuwa na kasoro mbalimbali, hivyo hutakiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya kuruhusiwa kutumika hapa nchini.

"Wahusika wanatakiwa kufanya marekebisho kwenye karakana zenu, hivyo ni jukumu la Shiriika kuhakikisha wadau wote kwenye sekta hii wanajua viwango vinavyopaswa kuzingatiwa katiika kutoa huduma hiyo". Amesema.

Aidha amewataka wadau hao kutumia fursa hiyo ukizingatia nchi inaendeleza miradi ya kimkakati ikiwemo uchimbaji wa gesi, ambapo itafikia wakati ambapo watakaofanikiwa kutoa huduma katika miradi hiyo ni zile karakana zilizothibitisha mifumo yao kulingana na viiwango husika.

Amesema Shirika linaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa hapa nchiini zinakidhi matakwa ya ubora ikiwemo vipuri vya magari na karakana zinazotumia vipuri hivyo ili biashara iiwe inafanywa katika mifumo inayotolewa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments