TAASISI YA COMMUNITY HANDS FOUNDATION YATOA ELIMU YA AFYA NA MAADILI KWA SHULE YA MSINGIZI MCHIKICHINI 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Community Hands Foundation Bw.Paul Makoe akizungumza na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimika uliozinduliwa leo katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem, Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam Mkuu wa Shule ya Msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Jijini Dar es Salaam akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimika uliozinduliwa leo katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem, Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam Mtaalamu wa Afya Dkt.Jesse Mbako akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini iliyopo Mbagala wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimika uliozinduliwa leo katika shule hiyo iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam Wanafunzi wa shule ya msingi ya Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem, Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam wakimsikiliza mtaalamu (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimika uliozinduliwa leo katika shule hiyo. Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Jijini Dar es Salaam akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa shule hiyo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimika uliozinduliwa leo katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem, Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Wadau wa maendeleo nchini wameombwa kujitokeza kuunga mkono juhudi za maendeleo ya jamii kwa kuleta suluhu za matatizo yanayoikabili ikiwemo kutoa mafunzo ya afya, maadili na elimu kwa watoto na vijana.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Community Hands Foundation, Bw.Paul Makoe wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimika uliozinduliwa leo katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem, Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam yenye lengo la kuwafundisha watoto na vijana kuhusu afya, maadili na Malezi.

Amesema kuwa lengo la uzinduzi wa Mradi huo ni kutokana na tafiti ndogo waliyofanya na kukutana na malalamiko kutoka kwa Walimu na walezi ya uwepo wa upotovu wa maadili kwa wanafunzi hivyo kuja na mpango wa utoaji wa elimu hiyo.

"Mradi huu ni wa miaka mitano na tunatarajia kufikia zaidi ya Mikoa 20 ya Tanzania hivyo tunaomba wadau na taasisi nyingine kujitokeza kuunga mkono juhudi hizi tunazozitoa kuhakikisha jamii inapata uelewa kamili". Amesema Bw.Makoe.

Aidha amesema kuwa kama wanafunzi na vijana wakipatiwa elimu hiyo na kuitatua itawasaidia kukabiliana na magonjwa na maisha ya kila siku yanayozunguka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shule ya Mchikichini Bw.Bonifance Njavike amesema kuwa ujio wa taasisi hiyo utaleta manufaa hivyo itasaidia watoto katika makuzi yao hasa ya kimaadili.

Naye Mjumbe wa kamati ya shule ya Mchikichini Bi.Elizabeth George amesema kuwa utolewaji wa elimu hiyo imekuja muda muafaka hivyo itasaidia Watoto kutokuwa na malezi mabaya.

Awali akizungumza Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mchikichini Mwl.Erenest Kibwinya ameishukuru Taasisi hiyo kwa hatua ya utolewaji wa elimu hiyo na kuomba taasisi zingine kuiga mfano huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments