SIMBA SC YAICHAPA RED ARROWS FC MABAO 3-0 KOMBE LA SHIRIKISHO

 


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Simba Sc imefanikiwa kuwachapa Red Arrows Fc ya nchini Zambia kwa mabao 3- katika mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanjja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Licha ya uwanja kujaa maji Simba Sc ilicheza kandanda safi na kufanikiwa kuondoka mapumziko wakiwwa na faida ya mabao mawili yaliyofungwa na Benard Morrison pamoja na Meddie Kagere.

Kipindi cha pili kilianza Simba Sc ikionekana bado inahitaji magoli zaidi licha jya kuwa mbele kwa mabao mawili ambapo dakika 79 ilifanikiwa kupata bao  la tatu kupitia tena kwa nyota wao Benard Morrison .

Simba inahitaji ushindi wowote ama sare katika mchezo ujao ili waweze kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho ambapo Red Arrows watakuwaa nyumbani kwenye mchezo huo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments