MSALALA WAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA....JAMII YATAKIWA KUEPUKA KUMALIZA KESI KIENYEJI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, November 26, 2021

MSALALA WAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA....JAMII YATAKIWA KUEPUKA KUMALIZA KESI KIENYEJI

Wana Mabadiliko wakiwa wamebeba bango linaloonesha mfumo wa maisha ya mwanamke katika familia na jamii wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jamii imetakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi panapotokea matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kutoa ushahidi mahakamani badala ya kumaliza kesi kienyeji ili kuwezesha kufikiwa kwa maamuzi ya kimahakama yanayolenga kukomesha matukio ya ukatili katika jamii.

Hayo yamebainishwa Novemba 25,2021 wakati uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala yaliyofanyika kwenye kata ya Lunguya mkoani Shinyanga yakiongozwa na kauli mbiu ‘Ewe Mwananchi Komesha Ukatili wa Kijinsia Sasa’.

Kupitia uzinduzi huo wa Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala wametakiwa kuacha tabia ya kumaliza kesi kifamilia bila kulishirikisha jeshi la polisi hali inayosababisha kuendelea kutokea kwa matukio hayo.

Akitoa taarifa za mwenendo na matukio ya ukatili katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, Msaidizi wa Mkuu wa Upelelzi Halmashauri ya Msalala Inspekta Costantine Challe amesema matukio ya ukatili wa kijinsia katika halimashauri hiyo yamepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na takwimu za miaka ya nyuma.

“Tunatoa wito sisi kama jeshi la polisi kuacha kabisa kupeana ng’ombe au kushawishiana katika maeneo ya kaya zenu na kumalizia kesi zenu huko, kesi zote naomba ziende kituo cha polisi lakini pia tunaomba mtoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili hizo kesi ziende mbele kwani jeshi la polisi pamoja na ninyi lengo letu ni moja tu kupambana na ukatili”, amesema Challe.

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi Benedicto Manwali ambaye ni Diwani wa kata ya Lunguya ameitaka jamii kuutambua mchango wa wanawake katika shughuli za maendeleo katika jamii na kwa ngazi ya familia.

“Niwapongeze TGNP kwa kuendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa jamii na ni imani yangu kuwa ukatili huu utatoweka kabisa hapo baadae. Ni vyema tukatambua kuwa familia yenye maendeleo inatakiwa mama awepo kwani ni mchangiaji mzuri wa shughuli za maendeleo”,amesema Manwali.

“Vituo vya taarifa na maarifa kwa kushirikiana na hawa wasaidizi wa kisheria katika kata zetu wanafanya kazi nzuri ya kupinga matukio ya ukatili. Natoa wito kwa wanawake mkifanyiwa matukio ya ukatili msirudi nyuma endeleeni kutoa taarifa za matukio ya ukatili”,amesema Manwali.

Aidha amelipongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wana jamii kupunguza matukio ya ukatili ikiwemo mauaji ya vikongwe akisema matukio hayo yamepungua ukilinganisha na hapo awali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga John Shija ameomba kuwepo kwa utaratibu maalumu utakaosaidia kupatikana kwa takwimu za matukio ya ukatili serikalini tofauti na hali ilivyo sasa.

“Kwa uzoefu wa shughuli ambazo zinaonekana zinafanyika ukiangalia takwimu hizi zimesambaa, tunaona takwimu za polisi,takwimu za Vituo vya taarifa na maarifa na takwimu za wasaidizi wa kisheria. Ombi langu ni kwamba tuwe na njia moja ya kupata takwimu zilizo sahihi leo hapa tungekuwa na takwimu moja ingetupa dira nzuri hivyo ni vizuri tukatengeneza mlango mmoja ambao utatusaidia kupata takwimu za halmashauri zinazohusu matukio ya ukatili wa kijinsia”,amesema Shija.

Katibu Msaidizi wa kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Mbunge amesema bado jamii haijaona umuhimu wa kusomesha mtoto wa kike ambapo baadhi ya wazazi wanaona watoto wa kike ni kama fursa ya kupata mali ikiwemo ng'ombe na wengine wamekuwa wakithubutu hadi kuwashawishi watoto wao wafeli kwenye mitihani ili waolewe.

Hata hivyo amesema vituo vya taarifa na maarifa vinaendelea kutoa elimu kwa jamii kuona umuhimu wa kupeleka watoto shule na kuelimisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni rasmi Diwani wa kata ya Lunguya Benedicto Manwali akizungumza Novemba 25,2021 wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala yaliyoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na UNFPA kwenye kata ya Lunguya mkoani Shinyanga 
Mgeni rasmi Diwani wa kata ya Lunguya Benedicto Manwali akizungumza Novemba 25,2021 wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala yaliyofanyika kwenye kata ya Lunguya mkoani Shinyanga yakiongozwa na kauli mbiu ‘Ewe Mwananchi Komesha Ukatili wa Kijinsia Sasa’.
Mwenyekiti wa Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga John Shija wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 

Mkuu wa Upelelezi Halmashauri ya Msalala Yohana Mafie  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Mkuu wa Upelelezi Halmashauri ya Msalala Yohana Mafie akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Msaidizi wa Mkuu wa Upelelzi Halmashauri ya Msalala Inspekta Costantine Challe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Katibu Msaidizi wa kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Mbunge akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Mwana mabadiliko akiwa amebeba bango lenye ujumbe 'Wanawake turuhusiwe kufuata mahari'  wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 

Mchezo wa  Igizo ukiendelea kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Igizo likiendelea kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

No comments:

Post a Comment

Pages