Breaking

Post Top Ad

Friday, November 12, 2021

NYUMBA YAWAKA MOTO WA AJABU MUSOMA..UNAUNGUZA MAGODORO, NGUO TU

Familia mmoja Manispaa ya Musoma Mkoani Mara imelazimika kulala nje kutokana na nyumba waliyokuwa wanaishi kuwaka moto wa ajabu ambao unaunguza Nguo,Magodoro na baadhi ya thamani za ndani huku ikiacha jengo la nyumba hilo bila madhara yoyote.

Mmoja wa wana familia amesema hawana maelezo ya kutosha kuelezea chanzo cha moto huo bali wako tayari kwa gharama yoyote kutafuta suluhu kwa yeyote anayehusika na moto huo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Longinus Tibishubwamu ameiomba familia hiyo kuondoka katika nyumba hiyo kwa muda ilikuondoa taharuki hiyo wakati uchunguzi wa kitalamu ukiendelea ilikuikoa familia hiyo.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages