MFANYAKAZI WA MUHIMBILI AFARIKI AKIVUTA KAMBA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, November 23, 2021

MFANYAKAZI WA MUHIMBILI AFARIKI AKIVUTA KAMBA


Mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Ally Lidengi amefariki uwanjani wakati akicheza mchezo wa kuvuta kamba kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Taasisi za Umma na sekta binafsi (SHIMMUTA) ambayo yanaendelea mjini Morogoro.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu hospital ya Taifa Muhimbili Daktari Prakseda Ogweyo amesema tukio hilo limetokea juzi Novemba 20,2021 katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo amesema marahemu huyo baada ya kuvuta kamba alianguka na alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Morogoro tayari alikutwa ameshafariki

Amesema kwa sasa mwili wa marehemu unasafrishwa kuelekea hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha kifo chake.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages