Breaking

Post Top Ad

Thursday, November 18, 2021

HATIMAYE P- SQUARE WAUNGANA TENA


HEADLINE kubwa ya entertainment Barani Afrika kwa sasa ni ile inayowahusu Kundi la muziki la P-SQUARE kutoka nchini Nigeria ambalo lilikuwa likiundwa na ndugu wawili Peter Okoye na Paul Okoye limerudi tena upya.

Hii ni baada ya usiku wa kuamkia leo, mapacha hao kukutana kwa mara nyingine baada ya kutengana tangu mwaka 2016 kutokana na ugomvi wa kifamilia licha ya kusuruhishwa mara kibao lakini wawili hao walikuwa wamegoma kabisa kupatana.

Tofauti hizo ziliisha tangu wiki iliyopita Peter alipoonekana akiwachukua watoto wa kaka yake Paul ambao wanaishi nchini Marekani na kuwapeleka shopping.

Baada ya mapacha hao kukutana, sasa wanarudi kama mwanzo ingawa bado haijaeleweka hata muziki wataanza kutoa pamoja au laah.

Katika video inayosambaa mitandaoni inamwonesha Peter akisalimiana na kaka yake mkubwa Jude ambaye ndio alikuwa meneja wao, na baadae kusalimiana na Paul kwa furaha kubwa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages