Breaking

Post Top Ad

Wednesday, November 3, 2021

MWANAMKE AMUUA KWA KISU MKE MWENZAKE Mwanamke mmoja Yvonne Wanjiru mkazi wa eneo la Subukia kaunti ya Nakuru nchini Kenya anadaiwa kumuua mke mwenza wake aitwaye Bernice Wangeci  kwa kumdunga kisu baada ya ugomvi kuzuka kati yao baada ya mume kumleta Bernice Wangeci nyumban kwa Yvonne. 

Mshukiwa Yvonne Wanjiru anasemekana kumvamia kwa kisu mke mwenza Bernice Wangeci ambaye alikuwa ameenda nyumbani kwa mumewe bila ya matarajio yake siku ya Jumanne, Novemba 2,2021.

Akidhibitisha kisa hicho, OCPD wa Subukia Patricia Nacio alisema Yvonne mwenye umri wa miaka 25 aliletewe mke mwenza Bernice na mumewe akiwa nyumbani.

Aidha, Nacio aliwaonya wanandoa dhidi ya kujichukulia sheria mikononi na kusababisha vifo vya kiholela.

 Baada ya kutelekeza kitendo hicho, Nacio alisema mshukiwa alitoroka na kwa sasa anasakwa na maafisa wa polisi.

Mwathiriwa Bernice alikimbizwa katika hospitali ya Subukia lakini alikata roho kabla ya kuhudumiwa na madaktari.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages