TANGAZO LA AJIRA: AFISA MASOKO NA MHUDUMU WA OFISI

Kampuni ya Kisena Group & Co. Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam ni kampuni iliyosajiliwa kisheria na inajishughulisha na shughuli mbalimbali kama Auctioneer, Cleaning na General Supply. 

 Inatangaza nafasi 3 za kazi. 

 A. Muda 

Muda wote ( full time ).

 B. Eneo la kazi : Dar es salaam.


 1. Nafasi 2 za Afisa masoko (marketing officers)

 Majukumu ya kazi. 

1. Kutafuta masoko ya kampuni.

2. Kuweka mpango kazi wa muda Mrefu na Mfupi wa kupata, na kutumia masoko ya kampuni.

3. Kutoa report za kila Wiki na Mwezi ama kulingana na maelekezo ya Ofisi, au pale zitakapo hitajika.

4. Kuongeza masoko na namna ya kusimamia masoko yaliyopo ndani ya kampuni.

5. Kazi nyingine kama zitakavyo pangwa ama kuelekezwa na kampuni.


 SIFA ZA MWOMBAJI

1.Awe na Shahada (Degree) ama Diploma ya masoko kutoka katika chuo kinachotambulika.

2. Awe na uwezo mzuri wa kuongea na kuandika Kiswahili na Kingereza.

3. Awe na uwezo wa kutumia kompyuta vizuri katika program za window.

4. Awe na uzoefu usiopungua angalau miezi sita.


 2.  NAFASI (1) Mhudumu wa ofisi ( office attendant)

 Majukumu ya kazi. 

Usafi wa ofisi.

Kufanya shughuli za secretary.

 Sifa za muombaji. 

1. Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea.

2. Awe na astashahada ( cheti) cha secretary au uhudumu wa ofisi.

3. Awe na uwezo wa kutumia kompyuta hasa kutuma na kupokea email, kupokea na kupiga simu.


 3. Viambatanisho

1. Kopi ya kitambulisho cha Taifa au cha mpiga Kura.

2. Kopi ya cheti cha kumaliza kidato cha nne au cha sita ama vyote kwa pamoja.

3. Cheti cha kumaliza mafunzo ya cheti au diploma.

4. Cheti cha kuzaliwa.

5. (CV) Wasifu unaoeleza kwa undani uzoefu na ujuzi wa mhusika kulingana na kazi anayoomba.


 MUHIMU 

Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kingereza au Kiswahili.

Mwisho wa kutuma Maombi ni 20/11/2021.

Maombi yote yatumwe kupitia 

Email ya kisenagroup@yahoo.com

Kwa maelezo zaidi piga simu.

0685638519

0763708284


Soma pia :

KISENA GROUP & COMPANY LIMITED 'KGC' WANAKUSANYA MADENI, TOZO, USHURU NA KODI ZOTE KWA UFANISI MKUBWA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post