WAZAZI WAASWA KUNYONYESHA WATOTO KWA MUDA WA MIEZI 6 ILI KUBORESHA LISHE KWA WATOTO

 Mratibu wa masuala la Lishe katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara Monica Ouk 

Na Frankius Cleophace - Tarime

Ili kujenga Misingi bora ya ukuaji wa mtoto pamoja na kuboresha suala la Lishe wazazi wameshauriwa kutumia vyema siku elfu moja ikiwa ni pamoja mtoto kunyonya maziwa ya mama kwa muda wa miezi Sita.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa masuala la Lishe katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara Monica Ouk wakati akizungumza kuelekea siku ya Lishe kitaifa ambayo ufanyika kila Oktoba 23 kila mwaka na mwaka huu  maadhiomisho yatafanyika Mkoani Tabora kitaifa.

 Monica alisema kuwa wazazi mara nyingi wamekuwa wakishindwa kunyonyesha watoto wao kwa kipindi cha Miezi sita kutokana kujikita kwernye majukumu kwa wingi jambo ambalo linaweza kuchangia suala la Udumavu.

Monica alisisitiza jamii kuendelea kufuata kanuni za lishe ili watoto waweze kukuwa na kustawi vizuri  ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kliniki pale wanapopata ujauzito mpaka wanajifungua.

“Suala la kunyonyesha maziwa ya Mama kwa mtoto ni muhimu sana pia mama anashauriwa kutumia vyakula vinavyopaswa kuboresha motto akiwa tumboni  ili kuweza kujenga mtoto”, alisema Monica.

Kauli Mbiu ya Mwaka huu katika kilele cha siku ya Lishe kitaifa inasema kuwa  “Lishe Bora ni Kinga Thabiti dhidi ya Magonjwa, Kula Mlo Kamili , Fanya Mazoezi, Kazi Iendelee.

Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa kwa mwaka huu ni ya pili tangu kuanzishwa kwake ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika Mwaka 2020 Mkoani Dodoma, ambapo siku hii imetajwa kutumika kama jukwaa muhimu katika kutekeleza na kuendeleza azma ya Serikali ya kutokomeza aina zote za utapiamlo nchini na kuongeza uelewa na ufahamu juu ya lishe bora na hatua madhubuti zinazopaswa kuchukuliwa na wananchi ili kuleta mabadiliko chanya hususani katika ngazi ya jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments