WATU WATANO WAUAWA WAKIJARIBU KUTEKA GARI LA POLISI KIGOMA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama

Watu watano wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na mabomu na mapanga wameuawa na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, wakati wakijaribu kuliteka gari la polisi lililokuwa likifanya doria katika barabara ya Kibondo- Kisulu eneo la Kibaoni karibu na kambi ya wakimbizi ya Nduta.

Taarifa ya tuki hilo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama, na kusema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kuwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi waonapo dalili za uhalifu.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments