TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAELEZA MBINU ZA UANDISHI WA HABARI ZA TAFITI ZA KISAYANSI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, October 8, 2021

TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAELEZA MBINU ZA UANDISHI WA HABARI ZA TAFITI ZA KISAYANSI

  Malunde       Friday, October 8, 2021


Mwezeshaji Dkt. Denis Mpagaze akitoa mafunzo kwa watafiti na Waandishi wa habari

Na Dinna Maningo, Mwanza
IMEELEZWA kuwa Mwandishi wa Habari akitumia mbinu nzuri za uandishi wa taarifa za tafiti za kisayansi zitawezesha wananchi kupata taarifa nyingi za utafiti za sayansi na taarifa hizo zitawavutia wasomaji na watazipenda kuzisoma jambo ambalo litasaidia jamii kuwa na uelewa mapana wa mambo ya taarifa za tafiti za sayansi na kuzitumia kufanya maamuzi mbalimbali.

Hayo yalielezwa na Dkt. Denis Mpagaze alipokuwa akitoa mada ya mbinu za uandishi wa habari za kitafiti wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa watafiti 15 na waandishi wa habari 25 kutoka mkoa wa Mara,Kagera na Mwanza, yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Mpagaze alitaja baadhi ya mbinu hizo kuwa ni pamoja na mwandishi kuhakikisha anakuwa na takwimu za kutosha kuhusu utafiti anaouripoti, kuuliza maswali kuhusu utafiti huo na ayatafutie majibu,vionjo katika taarifa,nukuu,matokeo ya utafiti,kuepuka vitisho unapofanya mahojiano na watafiti husika,kuepuka kuomba fedha kwa chanzo cha habari,mwandishi aipende taaluma yake.

"Usihukumu ,lazima uwe na notebook ya kuandikia taarifa, utafiti hauna muda kwamba unakimbizana kuwahi kutuma taarifa lazima uwe na muda wa kutosha wa kufanya tafiti wa taarifa za sayansi na wakuandaa habari,ujue utafiti unaosoma ni wa mwaka gani,kufahamu je huyo mtafiti nani kamfadhili kufanya utafiti au amefanya utafiti kwa maslahi ya mfadhili?", alisema Mpagaze.

Mpagaze aliongeza kuwa katika uandishi wa habari lazima mwandishi awe na mbinu za uandishi wa habari zitakazomvutia msomaji,kichwa cha habari kiwavutie wasomaji,aya ya kwanza iwe na uzito wa kumfanya msomaji kuzidi kuendelea kusoma habari iliyoandikwa,staili ya uandishi wa habari itamvutia msomaji kupenda kusoma taarifa za mwandishi.

"Unapopewa taarifa na mtafiti jaribu kwenda na kwa mtafiti mwingine ili ulinganishe tafiti zao,uliza maswali yote ambayo huyafahamu,mwandishi kuacha kuandika habari kisa chanzo cha habari kimekataa kuzungumza ni kosa, unatakiwa kuwa na mbinu na ushawishi kuhakikisha chanzo cha habari kinakupa taarifa",amesema.

Mbali na mada hiyo ya mbinu za uandishi wa habari za kitafiti,Mpagaze alifundisha nafasi ya mwandishi katika kuhabarisha habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (STU),namna yakuziba pengo la mawasiliano kati ya wanahabari na watafiti na majadiliano kwa njia ya vikundi.

Mwandishi kutoka chombo cha habari cha Sayansi na Teknolojia mkoani Mara Ajuaye Kabugu alisema kuwa mbinu hizo zitamsaidia kufanikisha habari zake za kitafiti kwakuwa awali hakuwa anazifahamu huku Stella Pantale mwandishi kutoka mkoa wa Kagera akisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemjenga na kumuhamasisha kupenda habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na kuahidi kuziandika kwakuwa tayali amepata mbinu za uandishi wa habari za tafiti.
Mwezeshaji Dkt. Denis Mpagaze akitoa mafunzo kwa watafiti na Waandishi wa habari
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post