Hukumu ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange Yaahirishwa | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 6, 2021

Hukumu ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange Yaahirishwa

  Malunde       Wednesday, October 6, 2021


Hukumu ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na aliyekuwa makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imekwama baada ya Aveva kushindwa kufika mahakamani.

Hukumu hiyo ilikuwa imepangwa kutolewa leo Jumatano, Oktoba 6, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu, Thomas Simba.

Hata hivyo kutokana na Aveva kutokuwepo mahakamani, mahakama hiyo imeshindwa kusoma hukumu hiyo na badala yake imeiahirsha hadi Oktoba 21, mwaka huu.

Kaburu ambaye ndiye pekee aliyefika mahakamani kusikiliza hukumu hiyo ameieleza mahakama hiyo kuwa Aveva ameshindwa kufika kuwa yuko hospitalini kwa ajili ya kliniki.
Kaburu amesema kuwa Aveva anahudhuria kliniki hiyo kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Hakimu Simba amekubaliana na maelezo hayo ya Kaburu na akaiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21, mwaka huu, saa 3:00 asubuhi kwa ajili ya kusomwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post