Breaking

Post Top Ad

Sunday, October 31, 2021

VIBOKO WA PABLO KUTAMBULIWA KISHERIA KAMA BINADAMUMahakama ya nchini Marekani imepitisha sheria ya kuwatambua Viboko waliokuwa wanamilikiwa na muuzaji hatari wa madawa ya kulevya nchini Kolombia, Pablo Escobar kama watu, kufuatia kesi dhidi ya Serikali ya nchi ya Kolombia juu ya kuwaua na kuwafanya viboko hao wawe tasa ili wasiweze kuzaliana zaidi nchini humo.

Viboko hao walipelekwa nchini Kolombia mwaka 1980 na Pablo Escobar ambaye alifariki mwaka 1993 , tangu hapo viboko hao hawakuwa na muangalizi hivyo kuzagaa ovyo na kuzaliana bila uangalizi. Ripoti zinasema kwa miaka nane viboko hao wameongezeka kutoka 35 hadi 80.

Makundi ya wanasayansi nchini Kolombia yametahadharisha hatari ya viboko hao kwa binadamu, sheria iliyopitishwa nchini Marekani juu ya kuwatambuwa Viboko kama binadamu inaweza isichukuliwe kwa uzito nchini Kolombia.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages