WILAYA YA ULANGA KUANDAA TAMASHA KUBWA LA KUHAMASISHA UWEKEZAJI


Mkuu wa Wilaya ya Ulanafa,Mhe Ngollo Malenya akizungumza mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu uwepo wa Tamasha la kuhamasisha wawekezaji katika Wilaya ya Ulanga litakalofanyika Oktoba 22 na 23 katika Uwanja wa Mapinduzi uliopo Mjini Mahenge,ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Mmoja wa Waratibu wa tamasha linalotarajia kufanyika Wilayani Ulanga .Michael Lyachema akifafanua baadhi ya mambo mbalimbali kuhusiana na tamasha hilo la kuhamasisha wawekezaji katika Wilaya ya Ulanga litakalofanyika Oktoba 22 na 23 katika Uwanja wa Mapinduzi uliopo Mjini Mahenge.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mhe.Ngollo Malenya alipkuwa akizungumza nao  jijini Dar es salaam
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

***


SERIKALI Wilayani Ulanga, Morogoro imetaja fursa tisa zinazopatikana katika Wilaya hiyo ambapo imetoa wito kwa watanzania kuzichangamkia katika kuwekeza na kufanya biashara.

Mwito huo umetolewa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Ngollo Malenya wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu uwepo wa Tamasha la kuhamasisha wawekezaji katika Wilaya ya Ulanga litakalofanyika Oktoba 22 na 23 katika Uwanja wa Mapinduzi uliopo Mjini Mahenge.

DC Malenya amesema lengo la tamasha hilo ni kutangaza fursa zilizopo wilayani humo pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza na kukuza pato la Taifa.

"Lengo la Tamasha hili la kuhamasisha uwekezaji katika Wilaya ya Ulanga linajulikana kama ULANGA IHEREPA, yaani AMAZING ULANGA, ULANGA KUNAPENDEZA, neno” Iherepa” lina maana inapendeza kwa lugha ya wenyeji wa Wilaya ya Ulanga WAPOGORO. Kauli mbiu ya Tamasha hili ni ‘‘TWENZETU ULANGA’’ Amesema DC Malenya

DC Malenya amesema pamoja na mambo mengine ya uwekezaji wanatarajia kuwa na michezo mbalimbali kama vile Riadha, kupanda milima (Hiking), Mbio za baiskeli (Mountain biking) pamoja na Ngoma za asili.

Aidha wageni kutoka ndani na nje ya nchi watapata fursa ya kutembelea maeneo ya vivutio ikiwa ni pamoja na utalii wa mazingira ya asilii, utalii wa majengo ya kihistoria, utalii wa hifadhi za misitu pamoja na kufanya utalii wa kuvua samaki.

Amezitaja fursa zilizopo katika Wilaya hiyo kuwa ni fursa katika sekta ya Madini, sekta ya kilimo na ufugaji, uzalishaji wa asali, utalii, uvuvi, ngoma za asili na majengo ya kihistoria.

" Wilaya yetu ina fursa za uwekezaji katika tafiti za madini, uchimbaji wa madini, ubia na wamiliki wa leseni za maeneo ya madini ambao wana leseni lakini hawana mitaji, vifaa na teknolojia ya uchimbaji wa madini. Aina ya madini yanayopatikana Wilayani Ulanga ni pamoja na Madini ya Kinywe (Graphites), Rubi na Dhahabu.

Wilaya ya Ulanga ina eneo lenye ukubwa wa hekta 1,068,889.43 ambapo kati ya hekta hizo ni hekta 269,775.34 ambazo sawa na 23.95% zinafaa kwa shughuli za kilimo na hekta 11,714 zinatumika kwa kilimo cha umwagiliaji," Amesema DC Malenya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments