Breaking

Post Top Ad

Monday, November 1, 2021

SHULE 10 BORA KITAIFA MATOKEO YA DARASA LA SABA .. SHULE 10 ZILIZOONGEZA UFAULU KWA KASI KUBWA


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2021 (Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2021... Hii hapa orodha ya shule 10 bora kitaifa na 10 ambazo zimeongeza ufaulu kwa kiasi kikubwa kitaifa miaka mitatu mfululizo.
Wakati matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa leo yakipokelewa kwa hisia tofauti, Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara ndiyo imeongoza kitaifa katika matokeo hayo huku Mkoa wa Kagera ukiongoza kuingiza shule nyingi katika orodha ya shule 10 bora kitaifa. 

Matokeo hayo ya mtihani huo uliofanyika Septemba mwaka huu yametangazwa Oktoba 30, 2021 na Baraza la Mtihani Tanzania (Necta) ambapo ufaulu wa ujumla umeongezeka kwa asilimia 6.6 ndani ya mwaka mmoja.

Watahiniwa 907,820 kati ya 1,107,460 waliofanya mtihani huo wamefaulu sawa na asilimia 81.97 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 74,130 ikilinganishwa na mwaka jana.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akitangaza matokeo hayo ameitaja Graiyaki ambayo ilikuwa na watahiniwa 50 kushika nafasi ya kwanza kitaifa ikifuatiwa na St Peter Claver ya mkoani Kagera katika nafasi ya pili.

Nafasi ya tatu imeenda kwa Shule ya Msingi Rocken Hill ya mkoani Sinyanga, Kemebos ya Kagera imeshika nafsi ya nne huku Bishop Caeser ya Kagera pia ikishika nafasi ya tano.
Shule ya Msingi Kwema Modern iliyokuwa na watahiniwa 44 ya Shinyanga iko nafasi ya sita, St Magret (Arusha) nafasi ya saba, Waja Springs (Geita) iko katika nafasi ya nane na Kadama ya Geita imeshika nafasi ya tisa.

10 bora hiyo imefungwa na Shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic ya mkoani Pwani.

Kwa matokeo hayo, mkoa wa Kagera ndiyo umeingiza shule nyingi (3) ukifuatiwa na Shinyanga na Geita ambayo imeingiza shule mbili kila moja huku mikoa iliyobaki ikiingiza shule moja moja. Pia orodha hiyo imetawaliwa na shule kutoka Kanda ya Ziwa ambapo nane za kanda hiyo zimeingia.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages