RUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI NA VYOMBO VYA WATOA HUDUMA ZA MAJI NGAZI YA JAMII KAHAMA..NDANYA ASISITIZA MAJI SAFI NA SALAMA


Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama , Timoth Ndanya akitoa hotuba katika mkutano wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA ) wa nusu mwaka mbele ya Wadau wa maji na Vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya Jamii mkutano huo uliofanyika Oktoba 29,2021 mjini Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Kahama.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama , Thimoth Ndanya ametoa wito kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kutoa elimu kwa jamii waweze kufahamu umuhimu wa kutumia maji safi na salama yalipo kwenye miradi wanayopelekewa na serikali na waondokane dhana potofu ya kuwa hayana radha nzuri.

Wito huo ameutoa Oktoba 29,2021 katika mkutano wa nusu mwaka wa wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wa wilaya ya Kahama uliofanyika mjini Kahama na kuwataka kuwapatia elimu waweze kutambua kutumia maji safi na salama yaliyopo katika miradi inayogharamiwa na serikali katika maeneo yao.

Alisema serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza miradi ya kuwapelekea huduma ya maji safi na salama kwa jamii lakini bado wanaendelea kuwa na dhana ya potofu ya kuendelea kutumia maji ya kwenye madimbwi kwa madai hayana radha nzuri kutokana na mazoea.

Ndanya alisema kamati za maji zilizopo katika miradi ya maji iliyokamilika kwa kushirikiana RUWASA kutoa elimu kwa jamii iweze kuondokana na mazoea hayo na waweze kujua umuhimu wa kutumia maji safi na salama kwa ajili ya afya yao na kuepuka na kupatwa na magonjwa mbalimbali ya milipoko.

Kaimu Meneja wa RUWASA wa wilaya ya Kahama ,Paschal Mnyeti akitoa taarifa ya miradi ya maji iliyotekelezwa katika kipindi cha nusu mwaka alisema serikali katika bajeti ya 2021 / 2022 imepanga kutumia kiasi cha shilingi 7,936,506,410.80 katika halmashauri tatu za Ushetu , Msalala na Manispaa ya Kahama.

Mnyeti akieleza mafanikio katika hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama vijijini katika maeneo ya miradi waliyotekeleza wilayani Kahama , alisema wamefanikiwa asilimia 64.4 sawa na kuwafikia watu wapatao 490,813 kati ya jumla ya wananchi 742,521 waishio sehemu mbalimbali huko katika vijijini.

Alisema RUWASA katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2019 hadi Oktoba 2021 miradi 16 ya usambazaji maji ya bomba imetekelezwa katika halmashauri zote tatu za wilaya ya Kahama kati ya hiyo 7 inatoa huduma na 9 ipo kwenye hatua mbalimbali ya utekelezaji .

Mnyeti alisema miradi hiyo inayotoa huduma kwa upande wa Manispaa ya Kahama upo kuna mradi mmoja wenye gharama ya sh.202 .7 milioni na unatoa huduma, Halmashauri ya Msalala miradi 7 yenye thamani ya shilingi 20 .228 bilioni inayotoa huduma ni mitatu na Halmashauri ya Ushetu ipo 6 ya sh.3.653 bilioni inayohudumia watu ni 4.

Kaimu Meneja wa RUWASA wa mkoa wa Shinyanga,Josephat Mkurya alisema changamoto katika miradi ya maji inayotekeleza katika maeneo mengi katika vijiji wilayani Kahama ni upatikanaji wa maji na radha yake katika visima vinavyochimbwa na wanaendelea kulifanyia kazi kwa weledi swala hilo na kuwataka wananchi kuendelea kutuza vyanzo vya maji.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama , Timoth Ndanya akitoa hotuba katika mkutano wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA ) wa nusu mwaka mbele ya Wadau wa maji na Vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya Jamii mkutano huo uliofanyika Oktoba 29,2021 mjini Kahama. Picha na Patrick Mabula
Kaimu Meneja wa RUWASA wa mkoa wa Shinyanga, Josephat Mkurya akiongea na viongozi na wajumbe na wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii kwenye mkutano wa nusu mwaka cha Julai 2019 hadi Oktoba 2021 uliofanyika wilayani Kahama.
Kaimu Meneja wa RUWASA wa wilaya ya Kahama Eng. Paschali Mnyeti akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa jamii ya vijijini kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Oktoba 2021.
Wajumbe, viongozi na wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wakiwa kwenye kikao hicho.

Wajumbe, viongozi na wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe, viongozi na wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe, viongozi na wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wakiwa kwenye kikao hicho
Wajumbe, viongozi na wadau wa maji na vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wakiwa kwenye kikao hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments