Breaking

Post Top Ad

Saturday, October 23, 2021

OBADIA AIBUKA MSHINDI SHINDANO LA MR. TANZANIA 2021


Obadia Okaman 

Na Andrew Chale, Dar es salaam

MTUNISHA misuli Obadia Okaman ametangazwa rasmi kushika taji la Mr. Tanzania 2021 katika shindano hilo lililiwakutanisha washiriki zaidi ya 20kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania. 

Usiku wa jana Umati uliojitokeza kwa wingi ndani ya Ubungo Plaza jijini Dar es salaam kushuhudia shindano hilo, ambapo walikuwa na wakati mgumu wa pamoja na Majaji juu ya Mr. Tanzania kutokana na wote kuwa na misuli mbavu nene lakini hadi saa sita na nusu usiku mshindi aliweza kutangazwa ambaye ni Obadia Okman.

Awali Obadia aliingia kwenye 10 bora na kisha kupenya  tatu bora dhidi ya wababe wengine akiwemo  Eric Majura ambaye ameshikilia taji la Mr Tanzania mara mbili mfululizo sambamba na Omary Lyombe.

Katika shindano hilo, Obadia alizawadiwa medali na kombe pamoja na cheti cha ushiriki huku akiondoka na hundi ya Tsh. Milioni 4 pamoja na seti ya kufungiwa king'amuzi cha DSTV chenye ofa maalum.

Mshindi wa pili Eric Majura aliondoka na kitita cha Milioni 2 huku mshindi wa tatu yeye akiondoka na hundi ya kitita cha Milioni moja.

Katika shindano hilo, washindi wote walionesha uwezo wao wa kutunisha misuli kwa njia tofauti huku mara zote wakipata shangwe kutoka kwa mashabiki waliojitokeza.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages