DKT. CHAULA AKABIDHIWA RASMI WIZARA YA HABARI

KATIBU Mkuu, Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas akimkabidhi baadhi ya vitendea kazi vya kitengo cha  Habari, Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula leo Jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya kitengo hicho.

 Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Katibu Mkuu  wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas amemkabidhi Ofisi ya Habari Katibu mkuu wa  Wizara Habari  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula huku akidai anasikia huzuni kuachana na Ofisi hiyo.

Hatua hii imekuja kufuatia hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko kwa kuihamisha idara ya HABARI kwenda Wizara ya Mawasiliano na teknolojia ya Habari hivyo wizara hiyo kuitwa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Dkt. Abbas amesema mabadiliko hayo yamelenga  kuongeza zaidi nguvu kwenye sekta ya wizara hizo mbili huku akiweka bayana kuwa anaiacha Ofisi hiyo  ikiwa na wafanyakazi 37  na vifaa mbalimbali muhimu kwa ajili ya utekelezaji majukumu.

"Nasikia huzuni kuondoka, nilizoea,naondoka nikiamini ufanisi utaongezeka,wakati naanza hakukuwa na gari lakini sasa naondoka nikiwa naacha magari manne ,kitengo hiki kina  Ofisi mbili Dar Es Salaam na Dodoma,"amesema.

Mbali na hayo Dkt. Abbas ameeleza kuwa sekta  ya habari ina mafanikio makubwa ambapo kwa sasa ina magazeti yaliyosajiliwa  270 ,Televisheni  51,Radio 298, Televisheni mtandao 496 na  Radio mtandao 500.

"Namkabidhi Idara ya hii nikiwa na matumaini kuwa  maboresho zaidi yatafanywa  kuleta tija," ameeleza Dkt.Abbas.

Aidha ameeleza mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta hiyo kuwa yamepatikana kutokana na kanuni sita walizojiwekea ambazo ni kuhakikisha kuendelea kuweka mipango,kanuni  ya pili iliyotumika kuweka mageuzi ni kuweka mipango mikubwa ,kutekeleza mipango yote,kufanya kazi kwa ushirikiano,mawasiliano ya pamoja katika  kutatua kero na kumuachia mwenyezi Mungu yale yaliyo nje ya uwezo wao.

"Mafanikio yote yaliyopo yamepatikana kutokana  na kanuni hizi sita,tuliamini kuwa hakuna linalowezekana bila ushirikiano",amesisitiza.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Abbas ametumia nafasi hiyo kutoa wosia kwa tasnia ya Habari na kusema kuwa "Kuweni na wivu kulinda taaluma yenu kuanzia mavazi,elimu,wajibu na haki zenu,usahihi wa taarifa,kwa kuzingatia kanuni za maaidli usahihi,ukweli na umakini,"amesema.

Kwa upande wake Dkt. Zainab Chaula ameeleza kuwa Dkt. Abbas anaondoka akiwa ameacha mchango mkubwa . 

"Natambua utumishi wetu uzae matunda zaidi,naelewa tunafanya kazi na kupitia changamito nyingi,naahidi  nitafanya kwa kufuata kanuni zote hizo sita kwa maendeleo ya Wizara yangu", amesema.

Mbali na hayo amewata Wafanyakazi hao 37 wa Wizara hiyo kumpa ushirikiano na kufanya kazi kwa uadilifu na matokeo makubwa.

"Nakupongeza sana Dkt. Abbas na timu yako ,tunaingia na naahidi nitaboresha ulipoacha,changamoto zilizopo Mimi Kwa kushirikiana  na wenzangu tutazifanyia kazi lakini pia mafanikio yaliyopo tunayaendeleza,"amesisitiza Dkt. Chaula.

Hata hivyo amesisitiza kuwa kuna maboresho ambàyo yanapaswa kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuboresha jarida la Kitengo cha habari kutolewa kila mwezi.

"Hatuwezi kufanikisha haya bila Mawasiliano lazima tuwasiliane vizuri ili tufanikiwe,hatupaswi kusikika ndani ya Tanzania peke yake tunapaswa kwenda nje zaidi watu watujue,tutengeneze majarida yetu ya Wizara kwa lugha ya kiingereza na kishwahili,wizara zilete mafanikio yake sisi tuandike kupitia wizara yetu,"amesema.

"Lazima tujipime kwenye mipango yetu tupo wapi,malengo yetu lazina yatimie wananchi wanahitaji matokeo ya Uwajibikaji wa pamoja,nataka  nikiondoka niache alama",amesema.

Dkt.Abbas amesema ameacha magari manne Mimi nitaacha magari 200 hayo ndiyo mafanikio,"amesisitiza.

Aidha amewataka Waandishi wa habari  kutumia muda mwingi kuambizana mambo makubwa ya Serikali kuliko kuandika uongi na kwamba Tanzania,nchini ina mambo mazuri ambàyo hayajulikani hivyo ni wakati wa kuyatangaza Dunia ielewe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post