BABU WA MIAKA 105 AFUNGA NDOA TABORA

Mzee Tuma Kulilinda akiwa na mkewe Joice Kasago
****

Mapenzi hayaangalii umri!! Ndivyo unaweza kusema! Kutoka Nzega Mkoani Tabora Mzee aitwaye Tuma Kulilinda mwenye umri wa miaka 105 amefunga ndoa na mpenzi wake Joice Kasago mwenye umri wa miaka 85. 

Shangwe na nderemo zimetawala wakati Mzee Tuma Kulilinda mkazi wa kata ya Ubinga wilayani Nzega akifunga ndoa na mwenza wake Joice Kasago miaka 85 ambapo kabla ya kufunga ndoa waliishi na kupata watoto saba huku mzee Tuma akiwa na jumla ya watoto 23.

Mzee Tuma ambaye ni Malenga na Mganga wa tiba asilia amesema Mungu amemuangazia kutimiza ndoto yake ya kufunga ndoa.

Akitoa salamu zake za pongezi baada ya kufungisha ndoa hiyo nyumbani kwa mzee Tuma, Paroko Parokia ya Kristo Mfalme Kitangili Padri Arnold Malambwa amesema tukio hilo ni fundisho kuwa maisha ya dunia yanapita.
Mzee Tuma Kulilinda na Joice Kasago wakivalishana pete
Mzee Tuma Kulilinda akiwa na mkewe Joice Kasago
Mzee Tuma Kulilinda akiwa na mkewe Joice Kasago

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments