AHUKUMIWA KWENDA JELA KWA KUMPOROMOSHEA MATUSI JIRANI YAKE - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, September 24, 2021

AHUKUMIWA KWENDA JELA KWA KUMPOROMOSHEA MATUSI JIRANI YAKE

 

Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 ambaye alimtukana jirani yake atalipa faini ya KSh 10,000 au atatumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani. 

Emily Achieng alipatikana na hatia kisha kuhukumiwa katika mahakama ya Kibera baada ya kukiri mashtaka ya kumtusi Selina Akinyi kwa njia inayoweza kuvuruga amani.

 Alitenda kosa hilo katika eneo la Katwekera lililoko mtaa wa Kibera mnamo Septemba 9, 2021 ripoti ya Nairobi News ilisema. 

Mtuhumiwa anasemekana kusema maneno "nenda ukamfufue babako kutoka kaburini ili aniambie hapa alipata Ukimwi."

 Mahakama iliarifiwa kwamba kabla ya kisa hicho, Akinyi ambaye alikuwa akifanya usafi alimwaga maji yenye taka karibu na nyumba zao hatua mabyo ilimuudhi Achieng.

 Mabishano yaliibuka kabla ya Achieng kuanza kumrushia matusi Akinyi. 

Hata hivyo, Achieng aliiambia mahakama kwamba alijibu tu matusi ambayo Akinyi alimrushia wakati wa mabishano. 

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages