UJANGILI CHANZO CHA FARU KUTOWEKA HAPA NCHINI

 

Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini Herman Batiho akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya faru duniani ambapo ilifanyika kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo Same mkoani Kilimanjaro ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo.
Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini Herman Batiho akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya faru duniani ambapo ilifanyika kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo Same mkoani Kilimanjaro ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo.

 Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mtaalamu wa Spish kutoka Shirika la WWF Profesa Noah  Sitati  akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Kamishna Msaidiz wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi  Emanuel Moirana akizungumza 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Same Anastazia Tutuba akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo  wa kwanza kulia akipata maelezo wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini Herman Batiho
Faru wakiwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mkomazi 
Wageni wakifurahia utalii wa Faru kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi 
Faru wakinywa maji kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kama anavyoonekana
Sehemu ya wanafunzi waliojitkeza wakati wa maadhimisho ya siku ya faru Duniani
Sehemu ya wanafunzi waliojitkeza wakati wa maadhimisho ya siku ya faru Duniani

NA OSCAR ASSENGA ALIYEKUWA KILIMANJARO



SHUGHULI za Ujangili kwenye hifadhi na sababu za kiimani kuamini kipusa cha faru ni dawa vimetajwa kama sababu mojawapo iliyochangia wanyama hao kutokweka duniani na hapa nchini

Hayo yalisemwa juzi na Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini Herman Batiho wakati wa maadhimisho ya siku ya faru duniani ambapo ilifanyika kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo Same mkoani Kilimanjaro ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo.

Alisema katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi walikuwa na faru wengi na nchi kwa ujumla kutokana na shughuli za ujangili zilipelekea faru wengi kutoweka ikiwemo sababu za kiimani wanaamini kipusa za faru ni dawa ambayo kwake haamini anaamini lishe bora ndio inayotibu maradhi ndani ya mwili.

Kamisha huyo Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini alisema sababu nyengine ni uharibufu wa mazingira kutokana na shughuli za kibinadamu ambazo ni pamoja na ukataji wa miti ikiwemo kuongezeka kwa makazi na shughuli za kilimo.

“Lakini pia sababu nyengine ni ufugaji na uchomaji wa moto vyote ilipelekea kuharibu mazingira ambapo ni sehemu ya makazi kama faru na wanyama wengine wakiwemo Tembo ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi inayotokana na shughuli za kibinadamu ”Alisema

Aidha alisema shughuli za kibinadamu inawezeka isiwe ni mkomazi na athari zake inakuwa zinajitokeza kwenye maeneo ambayo faru wanaishi kwa jumla matatizo kama hayo ndio yamepelekea siku kama hiyo leo wameadhimisha kuona namna ya kupelekea elimu kuelimisha jamii kuweza kuwahifadhi wanyama hao.

“Kama shirika tunaamini kuhifadhi maeneo hayo kwa kushirikisha na jamii kwa kutoa elimu itawezesha kuwalinda wanyama hao na wengine ambao ni vuvutio vya utalii ndani ya nchi na tunaamini hatuwezi kuwalinda wanyama hao kwa njia ya mtutu wa bunduki njia pekee ni kushirkisha jamii na hilo ndio ambalo wanalifanya”Alisema

Hata hivyo alisema wao kama shirika wanaamini kwamba athari hizo sasa wataweza kupambana nazo kwa kushirikisha jamii kama shirika kwa kutumia sayansi na teknojia uzao wa faru utaendeleaa kuwepo .

Awali akizungumza wakati wa shehere hizo za Faru Duniani Mtaalamu wa Spish kutoka Shirika la WWF Profesa Noah Sitati alisema wao kama shirika wamechagua wilaya ya Same kama wilaya moja muhimu kufanya sherehe hizo wao wana nia kubwa na mkomazi ndio mana wapo hapo.

Alisema faru walikuwa wametokea mpaka sifuri lakini hivi sasa idadi yao wameanza kuongezeka huku akiishukuru Serikali na Tanapa kwa kazi kubwa walioyoifanya kuhakikisha wanaendelea kuongezeka nchini.

“Niwaambieni kwamba Afrika ina hazina ya faru kama Tanzania faru walikuwa karibu hifadhi zote lakini walitoweaa na serikali imeweza kuweka mikakati sasa faru wameanza kuongezeka na tumekubaliana pia kwamba tutafungua ofisi mkomazi tuweze kufanya kazi kwenye maeneo ya Kilimanjaro na Tanga”Alisema

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya faru Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo alianza kwa kuwahamasisha wananchi kuhakikisha wanatembelea utalii wa faru kwa sababu ni sehemu ambapo unaweza kupata pumziko lako.

Alisema kwa sababu wanapohamasisha utalii wa ndani wanatengeneza ajira kwa vijana na kukua kwenye uwezo wa lugha kwa sababu wanapata ajira ya moja kwa moja na kuwapeleka wageni Hifadhini na wakina mama wanaweza kutengeneza shanga na mashuka.

Alisema jambo jinbine ni ukosefu wa maji kwa wanyama na binadamu ambapo katika eneo hilo aliwashukuru Shirika la WWF kwa mkakati huo wa kuhakikisha kwenye hifadhi maji yanapatikana na mazingira ya wilaya ya Same na miti yanaharibiwa sana na kupelekea kupungua kwa upatikanaji wa maji

“Hivyo niwatake Halmashauri ya wilaya ya Same na wadau wengine wakiwemo WWF na TFS kuona namna nzuri ya kuwafundisha watu wetu kuwatika miti”Alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments