SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MAZINGIRA YA UTOAJI TAARIFA KWA WANANCHI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Monday, September 27, 2021

SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MAZINGIRA YA UTOAJI TAARIFA KWA WANANCHI


Na Magrethy Katengu_Dar es salaam

Ikiwa imesalia siku moja kuelekea siku ya maadhimisho ya kupata taarifa, Umoja wa asasi zinazotetea haki ya kupata taarifa (CoRI) umeziomba  taasisi zote za kiserikali na zisizo za kiserikali kuzingatia kifungu cha sheria yakikatiba ubara ya  18 ya haki ya kupata taarifa kama ilivyotungwa na bunge miaka  iliyopita.

wito huo umetolewa leo na CORI, ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya kimaifa ya siku ya haki ya kupata taarifa ambayo ni Septemba 28 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kitaifa itaadhimishwa Dar es salaam katika ukumbi wa kimataifa Mwalimu Kambarage Nyerere

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Umoja wa asasi zinazotetea haki ya kupata taarifa (CoRI) Kajubi Mukajanga wakati akitoa tamko la pamoja kuelekea siku hiyo amesema ni nusu muongo sasa tangu kupitishwa na bunge sheria ya haki kupata taarifa lakini utekelezaji wake ni hafifu kumekuwa matukio ya Waandishi wa habari wawapo katika majukumu yao mtoa habari kuhitaji aandikwe anavyotaka yeye.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Tahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema kila mtu anayo haki ya kutafuta,kupatiwa na kusambaza taarifa,katiba pia ina tamko la kimataifa la haki za binadamu kama sehemu ya maudhui yake likitamka uhuru wa maoni,kujieleza na kujumuika

"Tunataka kuteuliwa kwa maofisa watoa taarifa katika kila taasisi ya Umma wenye mamlaka na wajibu wa utoaji taarifa za mara kwa mara na zile zinazoombwa na mwananchi mmoja mmoja kama inavyotamkwa na kifungu cha 7cha sheria",alisema  Balile.

Hata hivyo amesema kuna umuhimu wa kuanzishwa mfumo wa ufuatiliaji kubaini maombi yote ya taarifa na majibu yake katika taasisi za Umma ili kuepusha malalamiko baadhi ya waandishi kuwa barua za maombi wanapohitaji taarifa kutojibiwa au kukaa muda mrefu bila majibu

Meneja utetezi kutoka twaweza Anna Rugamba amesema CoRI inaamini kuwa ipo haja ya marekebisho ya sheria ya huduma za vyombo vya habari ys mwaka 2016,kuongeza kasi ya Utekelezaji wa sheri haki ya kupata taarifa pamoja na maboresho na utekelezaji wa kanuni za sheria hizo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages