MAPACHA WAOA MKE MMOJA

Imezoeleka kuwa mara nyingi mapacha hupenda kuoa/kuolewa na mapacha wenzao lakini mambo yamekuwa tofauti kwa mapacha hawa ambao wamewaacha watu midomo wazi.

Hii ni baada ya ndugu wawili ambao ni mapacha wa kuzaliwa wamemuoa na kuishi naye kinyumba mwanamke mmoja.

Ndugu hao kutoka nchini Rwanda wamemuoa Mary Josaine na kuishi pamoja miaka miwili sasa. Mary anasema alianza mahusiano akiwa binti mdogo na mmoja wa mapacha hao lakini pacha huyo hakumwambia kama ana pacha mwenzake.

Siku moja akiwa kwenye harakati zake alikutana na pacha wa pili ambaye alimfuata na kuzungumza naye akidhani kwamba ndiye mpenzi wake wa siku zote.

Kijana yule hakukataa aliyapokea mapenzi ya binti huyo kwa moyo mmoja bila kujiuliza.

Walikwenda faragha na kushiriki naye tendo la ndoa akidhani ndiye barafu wa moyo wake, kumbe pacha wa mpenzi wake, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuwa na wapenzi wawili mapacha hao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments