BABA MZAZI AYACHOMA KWA JIWE LA MOTO MATITI YA BINTI YAKE



Polisi katika jimbo la Lagos nchini Nigeria wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyayachoma moto matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka nane kwa kutumia jiwe la moto.

Polisi wamesema kuwa baba huyo alitekeleza maasi dhidi ya binti yake, kwa sababu matiti yake yalikuwa yameanza kuonyesha ‘chuchu’, ambazo ni ishara za kwanza za kubalehe.

Taarifa zinasema mzazi wa binti huyo alitumia kumchoma mtoto wake kwa kumfunga jiwe la moto katikati ya matiti ya binti yake.

Kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikisema kuwa yuko katika hali mahututi, kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi Bw Banjo.

Baba yake msichana huyo aliripotiwa polisi na kikundi cha kutetea haki za watoto, na Msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos DSP Asijebotu amethibitisha madai hayo, akisema kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kulingana na taarifa nchini Nigeria, wazazi wa msichana huyo kwa sasa wanashikiliwa na polisi katika jimbo la Lagos.

Mkuu wa kikundi cha kutetea haki za watoto Comrade Ebenezer Omejalile, ambacho kilimshitaki baba huyo, amesema kwamba Bw Banjo , anayefahamika kama Panel, aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake .

“Baba wa msichana huyo alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake,” alisema.

Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake, na ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.

Mama wa msichana huyo alisema kuwa muwa wake alikuwa akimpiga binti yake mara kwa mara bila sababu za msingi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments