KATIBU MKUU WA CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA ZITTO KABWE - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Wednesday, September 8, 2021

KATIBU MKUU WA CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA ZITTO KABWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo  amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ndg. Zitto Kabwe.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 08 Septemba, 2021 Makao Makuu ya CCM Dodoma, ambapo Ndg. Zitto aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Ndg. Lawrence Malawa.

Pamoja na mambo mengine, Mazungumzo hayo yamelenga zaidi kujitambulisha kwa Mwenyekiti mpya wa TCD Ndg. Zitto Kabwe alieyechaguliwa mwezi Agosti mwaka huu.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari 
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages