ASKARI POLISI AFARIKI AKISHANGILIA MECHI YA SIMBA NA YANGA

.
Rashid Mohamed Jumaa enzi za uhai wake.
USHINDI walioupata Klabu ya Yanga wa bao 1-0 dhidi ya Klabu ya Simba na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa Ngao ya Jamii umesababisha kifo cha askari H.2636 Rashid Mohamed Jumaa.

Askari huyo alikuwa akifanya kazi katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na inaelezwa alifariki dunia saa 12 jioni alipokiwa akiangalia mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga maeneo ya Stendi ya mabasi ya Wilaya ya Mpwapwa.

Mtangane huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa mkoani Dar es Salaam ulikuwa ukioneshwa Live na kituo cha Luninga cha Azam TV ambao ndio waliopewa jukumu la kuonesha mechi za Ligi Kuu nchini.

Wakati askari huyo akishangalia na kuwa na furaha iliyopitiliza askari polisi huyo alianguka chini,hivyo alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ambapo baada ya kufikishwa hapo madaktari walithibitisha alishafariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa inayoelezea tukio cha kifo cha askari huyo inadai alikuwa shabiki wa kutupwa wa Yanga na ushindi wa bao 1- 0 ambao Yanga waliupata katika dakika ya 11 ya mchezo huo uliochezwa jana Septemba 25 mwaka huu 2021 kuanzia saa 11 jioni ndio unaodaiwa kusababisha kifo hicho.

Askari huyo aliyekuwa akifanya kazi katika Wilaya ya Mpwapwa ni mwenyeji wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Chanzo - Michuzi blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments