POLISI ARUSHA YANASA MTANDAO WA WIZI WA PIKIPIKI , RPC AWAITA WANANCHI 'CENTRAL'


Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sita wa wizi wa pikipiki baada kufanya operesheni katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine Masejo alisema Operesheni hiyo iliyoanza tarehe 12 Septemba 2021 ni endelevu. 

Kamanda Masejo alisema watuhumiwa watano walikamatwa jijini Arusha na mmoja alikamatwa katika maeneo ya Mto wa Mbu wilayani Monduli, huku mmoja wao ambaye ni mkazi wa Kwa Mrefu jijini Arusha alikutwa na pikipiki nne, kadi nane za pikipiki pamoja na mikataba ya mauziano. 

“Jumla ya Pikipiki zilizopatikana ni tisa ambazo ni Toyo yenye namba za usajili MC 201 ABB, Toyo Power yenye namba za usajili MC 816 BHX rangi nyeusi, Honda Daz yenye namba za usajili T. 744 AZP rangi nyeusi.

Zingine ni Kinglion yenye namba za usajili MC 763 CBU, Sinoray yenye namba za usajili MC 600 CBR, Kinglion nyekundu yenye namba za usajili MC. 783 CFW, Kinglion yenye namba za usajili MC 306 CGD, Sinoray yenye namba za usajili MC 492 BPZ na Sinoray yenye namba za usajili MC 718 CHU.”

Kamanda Masejo alibainisha kwamba, wakati wa mahojiano watuhumiwa hao walikiri kushiriki kutenda matukio hayo ya uhalifu mkoa hapa na kisha kuuza mikoa ya jirani.

Aidha kupitia taarifa hiyo, Kamanda Masejo amewaarifu wananchi walioibiwa Pikipiki kufika katika kituo kikuu cha Polisi Arusha wakiwa na viambatanisho  vya umiliki kwa nia ya kuzitambua.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa waendesha Pikipiki maarufu kwa jina la “Boda Boda” kuendelea kuchukua tahadhari za usalama wao na mali zao pindi wanapowahudumia abiria hasa nyakati za usiku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments