MAMA AMCHOMA MOTO MTOTO WAKE WA KIKE KISA KAOMBA FEDHA KWA MPITA NJIA



Na John Walter -Manyara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia mwanamke Janeth Dotto Vicent ambaye ni mkazi wa Mji wa Babati kwa tuhuma za kumchoma mtoto wake wa kike sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Marrison Mwakyoma amethibitisha leo Septemba 14,2021 ambapo amesema tukio hilo Septemba 12 mwaka huu saa tatu asubuhi katika mtaa wa Mrara Juu.

"Mtoto huyo wa miaka mitatu alichomwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali baada ya kuchukizwa na kitendo cha mtoto wake kuomba fedha kwa mpita njia,"amesema.

Kamanda Mwakyoma amesema kitendo hicho kilimfanya mama huyo kumchoma usoni na shingoni na kumsababishi majeraha ndipo wasamaria wema walivyoona kitendo hicho waliamua kutoa taarifa katika kituo cha polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo,kwa sasa mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati, Mrara akiendelea na matibabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments