DC MBONEKO AAHIDI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO STENDI ZA MABASI SHINYANGA



Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati wa ujenzi wa choo cha Mabasi yaendayo wilayani.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ameahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili wafanyabiashara pamoja na abiria, katika Stendi za Mabasi Mjini Shinyanga.

Mboneko amebainisha hayo leo, alipofanya ziara ya kutembelea Standi za Mabasi za Mjini Shinyanga ikiwamo Standi ya Wilaya ya Shinyanga na Stendi ya Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kuona maendeleo ya ukarabati wa vyoo, pamoja na majengo ya kupumzikia abiria.

Alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwenye standi hizo za Mabasi, ili wafanyabiashara wafanye biashara zao katika mazingira mazuri, pamoja na abiria kupumzika sehemu zenye kivuli wakati wakisubiri mabasi.

“Nimefanya ziara katika Standi za Mabasi kuona ukarabati ambao umefanyika wa ujenzi wa vyoo na majengo ya kupumzika abiria, na pale penye changamoto tutaendelea kuzitatua,”amesema Mboneko.

“Katika Stendi hii kuu ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga Ibinzamata, mbali na kukarabati choo hiki, pia tutajenga choo kingine kikubwa cha kisasa, kulikarabati jengo la kupumzikia abiria, pamoja na kufunga zinatumia umeme wa jua (Solar), ili usiku pawe na mwanga,”ameongeza.

Pia, amewataka wafanyabiashara wa Standi hizo mbili pamoja na abiria, kutunza usafi wa mazingira na kuacha kujisaidia haja ndogo kwenye makopo, bali wavitumie vyoo ambavyo vimejengwa na kuimarisha usafi.

Naye Mwenyekiti wa Standi ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga Ibinzamata Khobe Marwa, amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kukarabati choo cha Stendi hiyo, ambapo awali kilikuwa katika hali mbaya, lakini kwa sasa kipo katika mazingira mazuri na kulinda usalama wa afya zao.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na viongozi na wafanyabiashara katika Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Ibinzamata. Picha na Marco Maduhu

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua jengo la kupumzikia abiria katika Stendi ya Mabasi wilaya ya Shinyanga, ambalo linaendelea kupakwa rangi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati wa ujenzi wa choo cha Mabasi yaendayo wilayani.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati wa karo katika Stendi ya Mabasi ya wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati ujenzi wa choo cha Stendi ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga Ibinzamata.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati ujenzi wa choo cha Stendi ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga Ibinzamata.

Na Marco Maduhu-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments