HOUSE GIRL MBARONI KWA TUHUMA YA KUUA MTOTO WA BOSI WAKE ARUSHA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Monday, September 20, 2021

HOUSE GIRL MBARONI KWA TUHUMA YA KUUA MTOTO WA BOSI WAKE ARUSHA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo 

Na Abel Paul Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Msaidizi wa kazi za ndani (House Girl) jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka (13) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka minne aliyejulikana kwa jina la Natalia Essau.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo mtoto huyo amefariki dunia Septemba 17,2021  saa 09:00 mchana katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru katika halmashauri ya jiji la Arusha wakati akipatiwa matibabu baada ya kupigwa na House Girl.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha kifo cha mtoto huyo mwenye umri wa miaka minne ni baada ya kupigwa na msaidizi wa kazi za ndani (House girl) jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka (13) Mkazi wa moshono ambaye taarifa zimebaini miezi kadhaa iliyopita binti huyo aliajiriwa akitokea Mikoa ya Kanda ya Ziwa kuja Arusha kufanya kazi za usaidizi wa ndani",ameeleza Kamanda Masajo.

 Amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi.

Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi. 

"Nitoe wito kwa wazazi na waajiri ambao wanawachukua wasaidizi wa kazi za ndani kuhakikisha wanazingatia umri wa wasaidizi hao, vilevile kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya tabia zao kwa familia wanapotoka ili kuepusha madhara makubwa kama hayo yaliyojitokeza ambayo yamegharimu uhai mfano mtoto huyu mdogo.

"Pia niwaombe wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuzidi kuimarisha hali ya usalama kudhibiti uhalifu katika Mkoa wetu", amesema Kamanda Masejo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages