JAMAA ADAIWA KUWAUA WATOTO WAKE BAADA YA KUGOMBANA NA MKEWE


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 44 kutoka kijiji cha Bochura kaunti ya Kisii amedaiwa kuwauwa watoto wake wawili na kisha kujitoa uhai.

Kisa hicho kilithibitishwa na chifu wa kijiji hicho Lawrence Omar ambaye alisema Daniel Mosota aliwaua watoto wake wa miaka 5 na mwingine wa miaka saba kwa kuwakata kwa panga. 

Omar alisema  Mosota anadaiwa alikuwa amegombana na mkewe Naomi Nyaboke kabla ya kutekeleza kitendo hicho.

 Chifu huyo aliongezea kwamba Nyaboke alifanikiwa kukimbilia usalama wake Mosoto alipoanza kuwavamia ndani ya nyumba yao. 

Maafisa wa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua miili ya watatu hayo, imehifadhiwa katika mochwari ya hospitali ya rufaa ya Kisii ikisubiri kufanyiwa uchunguzi wa maiti.

Aidha, chifu huyo aliwarai wanandoa ambao wana mazoea ya kuzozana kila mara watafute ushauri kutoka kwa wataalam au viongozi wa kanisa badala ya kuuana kiholela.

CHANZO-  TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments