BETWAY YAZINDUA KITUO CHA KUSHUHUDIA MICHEZO TANZANIA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, September 12, 2021

BETWAY YAZINDUA KITUO CHA KUSHUHUDIA MICHEZO TANZANIA

 

Kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubashiri, Betway imechukua hatua kubwa katika kuongeza thamani kwenye sekta ya michezo nchini Tanzania.  Betway imezindua kituo cha kisasa cha kushuhudia michezo na kubashiri kistaarabu ‘Betway Sports Experience Center.’

Kituo hicho cha kipekee na cha aina yake ni sehemu itakayowakutanisha wapenzi wa michezo kushuhudia michezo mbalimbali na kufanya ubashiri katika mazingira ya kuvutia.

Kituo hiki ambacho kimepewa jina la Dimba la Betway kitakuwa pia ni kituo cha elimu kuhusu michezo na namna ya kubashiri kistaarabu. Kituo hicho kipo ndani ya ofisi za Betway zilizopo Mbezi Beach, Dar es salaam.

Eneo hili la Betway limewekewa vifaa vya kisasa ikiwemo simu janja na kompyuta maalumu kwa ajili ya wateja kujisajili na kufanya ubashiri wa michezo inayoendelea mubashara. 

Kituo hicho kimefungwa skrini maalumu za runinga zinazoonesha michezo mubashara inayochezwa kwa wakati huo na kutoa nafasi kwa wateja kufuatilia matokeo ya mechi hizo. Pia, kituo hicho kinatoa nafasi kwa wateja kucheza michezo ya kasino na michezo mingine ya ubashiri.

Ndani ya dimba la Betway mashabiki wa michezo watapata nafasi ya kukutana na kuwasiliana moja kwa moja na timu ya Betway kwa uhuru na katika mazingira mazuri zaidi.

 Pia, kituo hiki kinatoa nafasi ya wateja kuuliza maswali, kusajili akaunti mpya, na kufanya ubashiri kwa kutumia simu na kompyuta zilizopo ndani ya kituo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe alisema kuwa uzinduzi wa kituo hicho cha ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuongeza thamani katika sekta ya michezo nchini.

"Sisi (Betway) tuna furaha kubwa kuzindua kituo hiki cha kipekee na muhimu kwa mashabiki wa michezo nchini Tanzania kuweza kukutana na kufurahia kwa pamoja na kwenye mazingira ya kuvutia.

 Hii ni sehemu ya ahadi yetu - kuongeza thamani katika michezo ya kubashiri na sekta ya michezo kwa ujumla kwa sababu kituo hiki kitakuwa kama kitovu cha michezo ambapo mashabiki wataweza kukutana, kutazama michezo, na kufanya ubashiri wao kwa njia bora ambayo haijawahi kutokea hapo awali," alisema.

Akizungumza na wadau wa michezo pamoja na wanahabari waliohudhuria tukio la uzinduzi, Jimmy alisema kuwa Betway inafanya kazi kutimiza ahadi zake za kukuza maendeleo ya michezo nchini Tanzania kama ilivyoahidi wakati ikiingia nchini na kuwahakikishia wote kuwa Kampuni hiyo itaweza kuwaongoza wateja wake katika kuiishi na kuitimiza kauli mbiu ya "Bashiri Kistaarabu" kwa kuwaonyesha wateja wake kwa vitendo.

"Sisi Betway tunajivunia kuhamasisha wateja wetu wote kubashiri kistaarabu. Tutatumia kituo hiki kama kituo cha kuelimisha mashabiki wa michezo nchini Tanzania kuhakikisha wanaielewa na kuikubali dhana ya kubashiri kistaarabu. Tunawakaribisha mashabiki wa michezo kufika katika kituo hiki kujionea na kufurahia maana halisi ya michezo,'' aliongeza.

Kama sehemu ya hafla ya uzinduzi, wahudhuriaji walifurahia uchambuzi wa moja kwa moja wa michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyochezwa siku ya Jumamosi. 

Uchambuzi kutoka kwa wachambuzi maarufu wa michezo nchini Tanzania, Maulid Kitenge, na Edo Kumwembe uliwavutia mashabiki wadau waliohudhuria hafla hiyo. 

Wahudhuriaji pia walishiriki katika mashindano ya michezo kama vile utabiri wa matokeo na wafungaji wa mabao, na kuweza kujipatia zawadi mbalimbali kutoka Betway.

Michael Valentine, aliyejitambulisha kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United alikuwa ni moja ya waliohudhuria katika hafla hii na kueleza kuwa alijionea utofauti mkubwa katika kituo hicho cha Betway. Michael pia ameunga mkono hatua ya kampuni ya Betway kuwekeza nchini Tanzania na kuitaka iendelee kutoa huduma za kipekee. 

“Mimi ni shabiki mkubwa wa michezo, kwa muda mwingi nimekuwa nikiwaona Betway kwenye vyombo vya habari kupitia timu za ligi kuu ya Uingereza zinazofadhiliwa na Betway, na furaha kuona wamekuja nyumbani Tanzania,” alisema.

Pia, aliongeza kwa kusema “sijawahi kuona kituo kama hiki nchini, kituo hiki ni cha kwanza hapa Tanzania na natumaini kitachochea uwekezaji mkubwa zaidi kwenye sekta ya michezo, na mashabiki watafurahia sana Betway kuanzisha shughuli zake nchini”.

Kituo hiki cha Betway kitakuwa kikifunguliwa katika siku zote 7 za wiki kuanzia asubuhi saa 3:00 hadi 5:00 usiku.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

No comments:

Post a Comment

Pages