ALIPA FAINI YA MILIONI 5 BAADA YA KUNASWA GESTI AKIPAKUA ASALI YA MKE WA RAFIKI YAKE - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Thursday, September 30, 2021

ALIPA FAINI YA MILIONI 5 BAADA YA KUNASWA GESTI AKIPAKUA ASALI YA MKE WA RAFIKI YAKEMfanyabiashara wa duka la simu mkoani Katavi amemfumania rafiki yake  ambaye ni mfanyabiashara wa zao la mpunga katika Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele mkoani humo kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na mke wake wakihondomolana (wakivunja amri ya sita).

Taarifa zimeeleza kuwa baada ya jamaa huyo kufumaniwa, rafiki yake huyo alimtaka kumlipa faini ya pesa kiasi cha shilingi milioni 5, kiasi ambacho alikilipa bila pingamizi yoyote.

Kupitia mitandao ya kijamii kuna video inasambaa ikimuonesha jamaa alivyofumaniwa, na akisikika rafiki yake akizungumza kwa uchungu, kuhusu rafiki yake huyo kujihusisha kimapenzi na mke wake ambaye wamezaa mtoto mmoja.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages