MTOTO WA MIAKA MINNE ABAKWA KATAVI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 15, 2021

MTOTO WA MIAKA MINNE ABAKWA KATAVI

  Malunde       Wednesday, September 15, 2021

Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Neema Hussein Katavi
Mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye jina lake limehifadhiwa amebakwa na kijana aliyetambulika kwa jina moja la George, huko katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. 

Kwa maelezo ya mtoto huyo amesema kijana huyo alimchukua kwa lengo la kumpeleka dukani kumnunulia pipi na kisha kutokomea naye porini na kumfanyia ukatili huo.

Amesema baada ya kutekeleza ukatili huo alimrudisha mpaka maeneo ya jirani na nyumbani kisha kumwambia mtoto aende nyumbani na mhusika kukimbia kusikojulikana.

Akizungumza na Nipashe mama mdogo wa mtoto huyo (Jina linahifadhiwa), amesema mtoto huyo alipotea mazingira ya nyumbani baada ya kuulizia aliambiwa ameondoka na kijana huyo.

Amesema kijana huyo ni rafiki wa karibu na marehemu kaka yao hivyo alikuwa akienda mara kwa mara katika mji huo na walimchukulia kama mtoto katika familia hiyo.

Amesema baada ya mtoto huyo kurudi nyumbani alionekana kukosa raha na pia alikuwa amechoka sana alivyo taka kumuogesha ndipo aligundua baada ya kumuona sehemu yake ya haja kubwa ina kinyesi na damu.

Familia ya mtoto huyo wameliomba Jeshi la Polisi kumtafuta na kumchukulia hatua kijana aliefanya ukatili huo.

Kwa upande wao baadi ya majirani akiwemo, wamesema tukio hilo wamelisikia na kuiomba jamii iwalinde na kuwaangalia kwa ukaribu watoto wao ili kuepukana na vitendo hivyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Katibu wa Hospitali ya Rufaa mkoani Katavi Dk. Boniface Lyimo, amekiri kumpokea mtoto huyo na baada ya kumfanyia vipimo waligundua ni kweli ameingiliwa kinyume na maumbile baada ya kuona mabaki ya mbegu za kiume.

Chanzo - Nipashe
  Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
  logoblog

  Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

  Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
  https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
  Previous
  « Prev Post