BWANA HARUSI AVUNJIKA MGONGO BAADA YA MARAFIKI KUMRUSHA JUU, WAKAACHA KUMDAKA


Sherehe moja ya harusi imegeuka ajali baada ya bwana harusi mwenye umri wa miaka 31 kukimbizwa hospitalini kwa kuvunjika uti wa mgongo wake baada ya marafiki zake bwana harusi huyo kumrusha hewani na kuacha kumdaka wakimuacha akiangukia kichwa chake.

Kisa hicho kilitokea katika harusi moja kaunti ya Bihor, Kaskazini Magharibi mwa Romania wiki moja iliyopita ambapo Bwana harusi aligeuka kuwa mgonjwa katika hafla yake ya harusi baada ya kuangukia kichwa chake.

Kwa mujibu wa The Sun, bwana harusi huyo aliporushwa hewani mara ya kwanza, alidakwa lakini katika jaribio la pili aliangukia kichwa na kumsababishia jeraha baya.

Inaelezwa kuwa marafiki hao walimubeba haraka na kumuweka kwenye gari, hatua ambayo madaktari walisema ilifanya mambo kuwa baya zaidi. 

Video fupi iliyopakiwa kwenye YouTube na Short News inamuonyesha bwana harusi huyo akiangukia kichwa chake katika hali ya kushangaza.

Bwana harusi amewaza kuwashtaki marafiki zake Bijourjust iliripoti kuwa sherehe hiyo ya harusi iliendelea licha ya kisa hicho huku bibi harusi na familia zote zikiwaburudisha wageni.

Daktari wa hospitali ambapo bwana harusi huyo alipelekwa kwa matibabu alizungumzia hali yake akisema: "Mgonjwa aliumia uti wake wa mgongo. Anaendelea vizuri japo pole pole. Amelazwa katika chumba cha kufanya upasuaji wa kichwa na wiki ijayo atafanyiwa uchunguzi zaidi."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments