BIBI KIZEE AGEUKA BINTI 'PISI KALI' | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 17, 2021

BIBI KIZEE AGEUKA BINTI 'PISI KALI'

  Malunde       Friday, September 17, 2021


 Video moja ya bibi wa miaka 75 akipodolewa na kugeuka kuwa binti mrembo imewavutia wanamtandao.
 
Video hiyo imeibuka kwenye mitandao ya kijamii ambapo bikizee anaonyeshwa akipodolewa na kugeuka binti mchanga .

 Wanamtandao wengine walihoji kuwa vipodozi hivyo vilipita kiasi

Katika video hiyo, iliyopakiwa kwenye Instagram na @arewafamilyweddings, bibi huyo anaonyeshwa akiwa ameketi huku msanii mpodoaji akimfanyia miujiza usoni.

 Akipakia video hiyo, @arewafamilyweddings alisema:

"Mtashtuka kuona urembo huu baada ya kupakwa makeup"

Wanamtandao maoni Wanamtandao walijaa kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko ya bibi huyo. 

Baadhi ya wanamtandao walidai kuwa bado bibi huyo angali mrembo bila kujipodoa.

Msanii mpodoaji awafurahisha wengi kwa kumbadilisha bibi wa miaka 75  iliripotia awali kuwa msanii mpodoaji Priscilla Appiah, alimiminiwa sifa mtandaoni kwa kazi yake njema.

Msanii huyo mpodoaji alimbadilisha mama yake kuwa sweet 16 na kupachika picha hiyo kwenye Instagram akimtakia heri njema akitimiza umri wa miaka 75.

 Katika karne ya sasa, wasanii wapodoaji barani Afrika wamekuwa wakionyesha ubunifu wao, na kufanya miujiza. 

Iwapo picha zote mbili hazitalinganishwa, watu wengi watadhania kuwa ni watu wawili tofauti katika picha moja.

 Hii ndio sababu msanii huyo mpodoaji alibadilisha muonekano wa mama yake kabisa.

 Akizungumza katika mahojiano, msanii huyo alisema kazi hiyo ilimchukua muda wa saa moja kukamilisha.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post