WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUIBUA HABARI ZINAZOHUSU WATOTO

 

Na  Frankius Cleophace Mara.

 Katika kuelekea  siku ya kimataifa ya amani  waandishi wa Habari  Mkoani Mara wameaswa kuendelea kuibua habari zinazohusu watoto wadogo kuanzia umri wa miaka sifuri hadi nane ili waweze kukua na kupata malezi bora.

 Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani  Mara Raphael Okello  wakati wa mahojiano  maalum kuelekea kilele cha  siku ya amani Kimataifa ambapo nchini Tanzania maadhimisho hayo kilele chake kinafanyika Jijini leo Dodoma.

Okelo alisema kuwa watoto wamekuwa wakitelekezwa na wazazi wao hivyo sasa ni jukumu la waandishi wa habari kuendelea kuibua habari hizo na changamoto ili ziweze kutatuliwa mapema.

 “Tunazungumzia suala la Amani, amani hawezi kuwepo wakati watoto wadogo wasiokuwa na hatia wanazaliwa wanatelekezwa hivyo sasa waandishi wa habari tukiungana na serikali katika kuibua masuala hayo na kutoa taarifa mapema ili watoto wapate malezi bora itasaidia kwa kiasi kikubwa”, alisema Okello.

 Vile vile Okello alisisitiza wazazi na walezi kuendelea kulinda na kulea watoto katika maadili mema ikiwa ni pamoja na kuwapeleka shule  watoto wote ili waweze kupata elimu bila kubagua hali zao.

“Kuna watoto pia ambao wanazaliwa na ulemavu hawapelekwi shule hivyo sasa jamii iungane kwa pamoja kwa lengo la kutoa haki  sawa” alisema Okello.

 Kwa upande wake Valerian Mgani kutoka shirika la ATFGM Masanga aliongeza kuwa suala la malezi na makuzi ni jukumu la wazazi wote hivyo kuelekea kilele cha siku ya amani wazazi waendelee kutoa malezi bora watoto wao.

“Pia nasisitiza  watanzania kuendelea kudumisha suala la amani ili kuendelea kutimiza majukumu yetu kwa sababu bila amani hakuna kitakachofanyika pia uchumi utuayumba”, alisema Valerian.

Maadhimisho ya siku ya amani kimatiafa hufanyika September 21  kila mwaka ambapo mwaka huu kauli mbiu inasema kuwa  "Kujikwamua zaidi  katika dunia  yenye usawa  zaidi"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments